NAIBU WAZIRI KATAMBI ATOA MAAGIZO KWA WAAJIRI NA VIONGOZI WA MATAWI TUGHE.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi ,Vijana,Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe Probas Katambi akizungumza kwenye kikao cha Tughe.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea

Na Mwandishi wetu, MWANZA

Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi ,Vijana,Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe Probass Katambi amewataka Viongozi wa matawi Tughe kuhakikisha wanatoa Elimu juu ya mafao kwa watumishi wastaafu kabla ya kustaafu.

Mhe. Katambi ameyasema hayo jijini Mwanza alipokuwa akifungua semina ya waajiri na viongozi wa matawi ya TUGHE iliyolenga kuondoa changamoto zisizo na tija mahala pa kazi.

Katambi alisema kuwa changamoto za wastaafu nyingi zinazotokea baada ya kustaafu serikalini, zinatokana na uelewa mdogo pamoja na uwajibikaji duni.

Katika ufunguzi wa semina hiyo,Naibu Waziri pia ameingeza kuwa Mwajiri asipoitisha vikao vya baraza la wafanyakazi kwa mujibu wa sheria TUGHE, wizara ipatiwe taarifa ili ifuatilie na kubaini sababu ya ukiukwaji huo.

“Nawashangaa sana wanao hujumu mahala pa kazi wakijua wanaikomoa serikali hapana ni wanahatarisha nafasi zao za ajira,sioni sababu za kuvujisha siri za ofisi kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa kwajili ya taifa letu”. Aliongeza Mhe. Katambi.

Aidha Waziri aliwaagiza kuwa mafunzo watayopata wayatumie ipasavyo katika kuendesha mabaraza ya wafanyakazi yenye tija.

“Hakikisheni mnashauri ipasavyo waajiri wenu ili kuondoa tabia ya ukiukaji wa sheria na kanuni zinazounda mabaraza ya wafanyakazi , kila taasisi ya umma iwe na Baraza la wafanyakazi linalofanya vikao vyake kwa mujibu wa sheria”. Amesema Mhe. Katambi.

Sambamba na hayo Naibu waziri Katambi amewapongeza Viongozi wa matawi Tughe kwa kuitisha semina hiyo kwani jambo hilo litakuwa na tija na masilahi mapana kwa serikali na taasisi zote .

“Kwa yale mtakayo kubaliana hapa na kuyajadili kwa pamoja yatatusaidia sana kutika kutafuta fursa Zaidi na kubadilisha changamoto kuwa fursa, haki na wajibu wa mwajiri uko upande pia ya mwajiriwa haki ya mwajiri ni wajibu wa mwajiriwa na wajibu wa mwajiriwa ni haki ya mwajiri”. Amesema Waziri Katambi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464