KAMATI YA UKUSANYAJI MAPATO YATEMBELEA MIRADI YA MANISPAA YA SHINYANGA INAYOTEKELEZWA NA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI

Kamanti ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikitembelea shamba la uwezeshaji vikundi kiuchumi lililopo Mtaa wa Azimio Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KAMATI ya ukusanyaji Mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, imefanya ziara ya kutembelea na kuona utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inatekelezwa na fedha za mapato ya ndani vikiwamo na vikundi vya Wajasiriamali ambavyo ni wanufaika wa mikopo ya asilimia 1o.

Kamati hiyo imefanya ziara hiyo leo Septemba 27, 2022, ambayo itachukua muda wa siku tatu na itahitimishwa Septemba 29,2022 chini ya Mwenyekiti wake Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Katibu wa Kamati hiyo Dk, Kulwa Meshack, akizungumza wakati wa ziara hiyo, amesema wameridhishwa na miradi ambayo inatekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia fedha za Mapato ya ndani, huku akibainisha kuwa tathimini kamili na mapendekezo watayatoa siku ya kuhitimisha ziara hiyo.

Aidha, akizungumza mara baada ya kutembelea vikundi vya wajasiriamali ambao ni wanufaika wa mikopo ya Halmashauri asilimia 10, ambayo nne kwa wanawake na vijana na mbili kwa watu wenye ulemavu, amewataka waitumie vizuri mikopo hiyo na kuinuka kiuchumi.

“Wajasiriamali ambao mmenufaika na mikopo hii ya Halmashauri asilimia 10 kupitia fedha za mapato ya ndani, mzitumie vizuri kujikwamua kiuchumi, pamoja na kuirejesha mikopo hiyo kwa wakati ili vikundi vingine navyo vikope,”amesema Dk. Meshack.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, amesema wamefanya ziara ya kuitembeza Kamati hiyo ili kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa kupitia fedha za mapato ya ndani.

Amesema Manispaa hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwa sasa kwenye ukusanyaji wa mapato yake ya ndani, kupitia mchango mkubwa wa kamati hiyo.

Kamati hiyo imetembelea Mashamba ya uwezeshaji vikundi kiuchumi, ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Bugweto kupitia fedha za mapato ya ndani, kikundi cha Wajasiriamali cha kutegeneza Sabuni za Magwanji, kikundi cha kutengeneza Magodoro, kikundi cha mashine za kusaga nafaka, pamoja na kushuhudia makabidhiano ya mfano wa hundi Sh.milioni 156.4 kwa vikundi 11 vya ujasiriamali.

Mwenyekiti wa Kamati ya ukusanyaji Mapato halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga , ambaye pi ni Meya wa Manispaa hiyo Elias Masumbuko akizungumza kwenye ziara hiyo.

Katibu wa Kamati ya ukusanyaji Mapato halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dk, Kulwa Meshack akizungumza kwenye ziara hiyo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye ziara hiyo.

Wajumbe wakiwa katika Shamba la uwezeshaji vikundi kiuchumi Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga, ambalo lilinunuliwa na Manispaa hiyo kupitia fedha za mapato ya ndani.

Ziara kwenye shamba la uwezeshaji vikundi kiuchumi ikiendelea.

Ziara kwenye shamba la uwezeshaji vikundi kiuchumi ikiendelea.

Muonekano wa baadhi ya maeneo ya shamba la uwezeshaji vikundi kiuchumi.

Wajumbe wakiwa kwenye kikundi cha utengenezaji wa Sabuni za Gwanji ambao ni wanufaika wa mkopo Sh.milioni 20 kupitia fedha za mapato ya ndani asilimia 10.

Wajumbe wakiangalia namna Sabuni za Magwanji zinavyotengenezwa.

Wajumbe wakiangalia Sabuni za Gwanji.

Wajumbe wakiwa kwenye kikundi cha utengenezaji wa Magodoro ambao ni wanufaika wa mkopo sh. milioni 40 kupitia fedha za mapato ya ndani asilimia 10.

Wajumbe wakiwa kwenye kikundi cha utengenezaji wa Magodoro.

Wajumbe wakiangalia ubora wa Magodoro.

Wajumbe wakiwa katika ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Lubaga.

Wajumbe wakiwa kwenye kiwanda cha kusaga na kukoboa nafaka Kitangili Manispaa ya Shinyanga ambao ni wanufaika wa mkopo wa halmashauri kupitia fedha za mapato ya ndani asilimia 10.

Ziara ikiendelea kwenye kiwanda kidogo cha kusaga na kukoboa nafaka.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa na wajumbe wa kamati ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakikabidhi mfano wa hundi Sh.milioni 156.4 kwa vikundi 11 vya ujasiriamali kupitia fedha za mapato ya ndani.

Makabidhiano ya mfano wa hundi kwa vikundi 11 vya ujasiriamali kupitia fedha za mapato ya ndani ya halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Sh.milioni 156.4
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464