Mwanafunzi kidato cha tatu ajiua kwa risasi Moshi, aacha ujumbe
Robert Meier (17) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari St Mary Goreti iliyopo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amejiua kwa kujipiga risasi huku akiacha ujumbe akitaka mwili wake uchomwe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa akizungumza na Mwananchi kwa simu baada ya kupata taarifa hizo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema lilitokea usiku wa kuamkia juzi.
Akisimulia tukio hilo, Kamnada huyo alidai kuwa kabla ya mwanafunzi huyo kujiua, aliacha ujumbe wa maandishi ulisomeka mwili wake uchomwe na majivu yake yasafirishwe kwenda Marekani yakazikwe pembezoni mwa kaburi la baba yake.
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.