MKUU wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akizungumza kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania CWT wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Na Kareny
Masasy, Kahama
Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga Festo Kiswaga ametoa maelekezo
kwa maafisa utumishi wa halmashauri kuhakikisha wanafuata utaratibu wa
kuwahisha taarifa za watumishi
wanaokaribia kustaafu na wale wanaotarajia kupanda madaraja kazini ili kuondoa ucheleweshaji wa stahiki zao.
Kiswaga
amesema hayo leo tarehe 23/09/2022 alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa
chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ulio wakutanisha
wajumbe takribani 250.
Kiswaga
amesema amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya ingawa kulikuwa na
changamoto ya mazingira ya kuishi wa walimu serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia
Suluhu imeanza kuyafanyia kazi na hata waliopandishwa madaraja wanalipwa stahiki zao .
Kiswaga
amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imetekeleza kwa kiasi kikubwa matakwa ya
walimu na kutoa maelekezo ikiwa maafisa utumishi wanatakiwa kuangalia wale wote wenye kukaribia
kustaafu kuwaandalia nyaraka zao mapema
ili kuondoa kero.
“Nimeambiwa
kuna watu ambao wako halmashauri ambao
wamekuwa wakichelewesha kuwapandisha
madaraja walimu sasa tunashughulika nao nakuchunguza kwanini wanachelewesha nanyi
walimu mkiwa na shida msikae kwenye
mabenchi kusubiri bali mpite moja kwa moja msikilizwe muwahi
kufundisha wanafunzi wetu”amesema Kiswaga.
Mwenyekiti
wa CWT mkoa wa Shinyanga Mathias
Balele amesema kuwa serikali
imefanya kazi kubwa kwa walimu kwani imeweza kuwajengea nyumba na mazingira ya
kufundishia kuwa mazuri huku upandishaji wa madaraja ukienda vizuri tofauti na
zamani.
Mwenyekiti
wa CWT wilaya ya Kahama Raymond Lutemba akiongoza mkutano huo kupitia taarifa ya
utendaji kazi kwa chama hicho kwa kipindi cha miaka miwili na nusu (March 2020 –
Septemba 2022) nakueleza kero mbalimbali wamezitatua ikiwemo uhamisho wa walimu
na wale bado mazungumzo yanaendelea na
waajiri wao.
Pia kulikuwa na ajenda ya
kuondokana na usafiri wa gari aina ya Coaster iliyokuwa ikibeba abira
25 hali ambayo walieleza inawapa
changamoto katika suala la usafirishaji
na kuwa bovu mara kwa mara.
Ambapo wajumbe wa mkutano huo walipendekeza kununuliwe gari aina ya TATA itakayobeba abiria 40 itakayosaidia katika kuwasafirisha wao wanapokuwa na shughuli mbalimbali .
Wajumbe wa mkutano mkuu wa CWT wilaya ya Kahama wakiwa katika sala kabla ya mkutano kuanza
Wageni waalikwa katika mkutano mkuu wa CWT wilaya ya Kahama wakiwa meza kuu
Katibu CWT wilaya ya Kahama Peter Gedi akitoa utangulizi katika mkutano mkuu wa chama hicho.
Mweyekiti wa CWT mkoa wa Shinyanga Mathias Balele akisalimiana na wajumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Kahama
Wajumbe wa mkutano mkuu wa CWT wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
Wajumbe wa mkutano mkuu wa CWT wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
wageni waalikwa wakiwa meza kuu ni mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga kushoto katikati ni Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Shinyanga Mathias Balele na upande wa kushoto ni kaimu katibu wa CWT mkoa wa Shinyanga Allen Shuri
Wajumbe wa kamati tendaji ya CWT mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa CWT wilaya ya Kahama Raymond Lutemba akiongea kwenye mkutano
Katibu wa CWT halmashauri ya Ushetu Alponnce Mbasa mgeni mwalikwa akisalimia wajumbe wa mkutano mkuu
Mwenyekiti wa CWT halmashauri ya Ushetu akisalimiana na wajumbe wa mkutano mkuu alipoalikwa CWT wilaya ya Kahama.
DK Baraka .C ,Kulwa Mkurugenzi wa hospitali ya CKM iliyopo Runzewe wilaya ya Bukombe mkoani Geita akiwa mdau wa elimu akihudhuria mkutano mkuu kwa kutoa salamu zake.