Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akiwataka wanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Nyawile akiwaeleza wasome kwa bidii baada ya kujengewa vyumba vya madarasa kwa fedha za tozo za miamala.
Na Kareny Masasy,
MKUU wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Festo Kiswaga amesema kuwa fedha za miamala ya tozo kiasi cha sh Millioni 537 .5 kilichopokelewa na halmashauri ya Msalala kimeweza kujenga miradi kwenye sekta ya afya na elimu.
Kiswaga
amesema hayo leo tarehe 10/09/2022 alipofanya ziara ya kutembelea miradi hiyo ambayo imekamilika kwa asilimia
100 na mingine kuanza kufanya kazi.
Moja ya
miradi aliyotembelewa ni shule ya
sekondari Nyawile iliyopo kata ya Kashishi ambayo imejengwa vyumba viwili vya madarasa kwa fedha za tozo
kiasi cha sh Millioni 25 nakuokoa
wanafunzi kutembelea umbali wa zaidi ya kilomita 20.
Pia Kiswaga
ameweza kutembelea kituo cha afya
Mwalugulu kilichopo kwenye
kata hiyo kilichotumia kiasi cha shilingi Millioni 500 kwa fedha za tozo ya miamala na ndani ya mwezi
huu kitaanza kufanya kazi.
Makamu mkuu
wa shule hiyo James Matiku amesema kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi
266 ilianzishwa mwaka 2021 ikiwa na vyumba vya madarasa viwili vilivyoanzishwa kwa nguvu za wananchi
na sasa vyumba vya madarasa viko tisa
vyote vimekamilika.
“Awali
walikuwa wakisomea shule ya sekondari ya
kata ya Bulige nakulazimika wanaoishi
maeneo ya kata ya Kashishi kutembea
umbali mrefu nakufikia wengine kutomaliza shule kwa kupata mimba na utoro wa
rejareja lakini sasa hali hiyo haipo tena wanapata na muda wa kujisomea”amesema
mwalimu Matiku..
Makamu
mwenyekiti wa halmashauri hiyo Flora Sagasaga
ambaye ndiye diwani wa kata ya Mwalugulu
amesema kuwa anashukuru kuwepo fedha za tozo za miamala kwani zimewasaidia kupata kituo
cha afya na majengo yote muhimu walikuwa na Zahanati pekee.
“ Wajawazito
na watoto walikuwa wakiteseka kwenda Hopsitali ya manispaa ya Kahama kupata
huduma umbali wa kilomita 30 hadi 40
lakini sasa watapata huduma hapa hapa kwani kuna jengo la wagonjwa wa nje (OPD)jengo
la mama na mtoto,jengo la upasuaji,jengo la kuchomea taka na maabara”amesema
Sagasaga.
Ofisa
mipango wa halmashauri ya Msalala Elikare Zabron amesema kuwa wamepokea kiasi
cha sh Millioni 537.5 kutoka serikalini fedha za tozo za
miamala na ulifanyika mgawanyo sekta ya afya sh Millioni 500 na sekta ya elimu sh
Millioni 37.5
‘Ambapo sh Millioni 25 zimejenga vyumba vya madarasa viwili Nyawile Sekondari,chumba kimoja sekondari ya Chela sh Millioni 12.5 na kituo cha afya kimoja cha Mwalugulu kiasi cha sh Millioni 500”amesema Zabron.
Chumba cha darasa kilichojengwa kikiwa kimekamilka na wanafunzi wameanza kusomea.
Wanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Nyawile iliyopo kata ya Kashishi halmashauri ya Msalala wakiwa darasani.
Ujenzi ukiendelea wa kituo cha afya kilichopo kata ya Mwalugulu kwa jengo la mama na mtoto..
Jengo la wagonjwa wagonjwa wa nje OPD katika kituo cha afya Mwalugulu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464