Na
Kareny Masasy, Msalala
HOSPITALI ya halmashauri ya Msalala imeanza kutoa baadhi ya huduma ikiwemo kliniki ya mama na mtoto na wagonjwa wa nje (OPD) ili kuwaepusha na kusafiri umbali mrefu kupata huduma.
Mganga mkuu
wa halmashauri hiyo dkt Ernest Chacha amesema hayo jana
hospitalini hapo nakueleza kuwa ujenzi wa hospitali hiyo
umegharimu sh Billioni 1.8 nakuwanufaisha wakazi takribani
500,000.
Dkt
Chacha amesema kuwa hospitali hiyo kuna jengo la wagonjwa wa
nje (OPD) Maabara,ICU,Mama na mtoto famasi, chumba cha kuhifadhia
maiti, chumba cha kuchomea taka pamoja na nyumba ya mtumishi.
“Kuanza
kufanya kazi hospitali hii kutapunguza safari za wagonjwa na wajawazito
wanaopewa rufaa kwenda manispaa ya Kahama kutoka kwenye Zahanati 36 zilizopo
kwenye halmashauri hii watatibiwa hapahapa”amesema dkt Chacha.
Dkt Chacha
amesema kuwa Kuna watumishi wa afya 57 na
katika hospitali hiyo wamepata watumishi wa afya 18 na fedha
za vifaa tiba na dawa kiasi cha sh Millioni 376 .
“Changamoto
iliyopo ni uhaba wa maji kwenye hospitali hiyo kutokana na
kukosekana kwa chanzo cha uhakika kwani ninaiomba
serikali kuharakisha mradi wa maji wa Nduku - Busangi chanzo
”amesema dkt Chacha..
Mganga
mfawidhi wa hospitali hiyo dkt Fredrick Macha amesema kuwa huduma
zilikuwa ni ngumu kutokana na uhaba wa vifaa tiba lakini
sasa mashine za mionzi zipo watumishi wapo wakutumia vifaa
vilivyopo.
“ Hospitali
hii imekamilika kilichosababisha kutoa huduma baadhi ni changamoto
ya uhaba wa maji kwani daktari wa upasuaji wapo,chumba cha
kujifungulia na wauguzi wapo” amesema dkt Macha.
Diwani wa
kata ya Ntobo iliyopo hospitali hiyo David Mlyandali amesema
kuwa hospitali kuanza kutoa huduma wamefarijika sana
wananchi walikuwa wakitumia gharama kubwa kumsafirisha mgonjwa.
Mlyandali
amesema kuwa changamoto ya ukosefu wa maji serikali
imeanza kulifanyia kazi licha ya hospitali pia wananchi nao wamekuwa
wakiteseka kwa kununua maji au kutumia maji ya visima vifupi.
Wakazi wa halmashauri ya Msalala Tabu Embasi na Clement Mihayo waliofika kupata huduma za afya katika hospitali hiyo wamesema kuwa kuanza kwa hospitali hiyo kumesaidia kwani wajawazito na wagonjwa wengine walikuwa wakipoteza maisha njiani kutokana na barabara kuwa mbovu na umbali kwenda manispaa Kahama.