KAMANDA WA POLISI MKOANI SHINYANGA AMESEMA VITENDO VYA KIKATILI VINALETWA NA RAMLI CHONGANISHI.




Kamanda wa  polisi mkoani Shinyanga  Janeth Magomi akiwa na kikosi cha Sungusungu   kata ya Mondo wilayani Kahama  kwa lengo la kutaka ushirikiano kwenye kufichua uhalifu na kuondoa vitendo vya kikatili.

Na Kareny Masasy,

KAMANDA wa polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi amesema kuwa ramli chonganishi zinazofanywa na baadhi ya waganga wa kienyeji ndiyo zinasababisha kuendelea kuwepo vitendo vya ukatili ndani ya jamii.

Kamanda Magomi amayasema hayo leo tarehe 15/09/2022  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mondo wilayani Kahama uliohudhuriwa na viongozi wa sungusungu kutoka vijiji vitano vya Sangilwa ,Penzi,Mwanzwagi,Mondo na Bumbiti.

Kamanda Magomi amesema kuwa hao waganga wa kienyeji waache ramli chonganishi kuna tukio moja limetokea Ushetu mzee kuuwawa kikatili lakini upelelezi ulivyofanyika ukabaini chanzo imani za kishirikina.

Kamanda Magomi amesema kuwa amekuja mkoa huu kwa muda mfupi amekutana na vitendo vya mauaji ya wazee,ubakwaji,mimba za utotoni na wivu wa mapenzi na vipigo kwa wanawake.

“Ninachowaomba ninyi sungusungu ndio mpo kwenye jamii vitendo vya uhalifu vikitokea mripoti mara moja kwenye jeshi la polisi kwani siku hizi sio kama zamani polisi kuogopeka tuna polisi jamii kila kata hivyo fichueni uhalifu ili tuweze kuutokomeza”amesema Kamanda Magomi.

Kamanda Magomi amewataka wanawake kutokaa kipya bali waeleze changamoto zao kwenye dawati la jinsia na wanaume nao wasijichukulie sheria mkononi hata kama wake zao wamewaudhi.

Mtemi wa sungusungu kata ya Mondo Pondamali Maziku amewataka wananchi kutofanya uhalifu kwani mila na desturi zao kaya inayofanya uhalifu hutengwa pia viongozi serikalini wasiwafumbie macho wahalifu pindi wanapokwenda kuwapa ripoti

Kikosi cha sungusungu kikitumbuiza katika mkutano wa hadhara kata ya Mondo wilayani Kahama


Kamanda wa polisi akisalimiana na viongozi wa sungusungu kata ya Mondo wilayani Kahama.



Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga akiwa na maafisa wa jeshi hilo kutoka wilayani Kahama


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akiwa na  mkuu wa oparesheni wilayani Kahama  Domisian  Mkungu  wakilipokea jeshi la sungusungu.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi  kushoto kwake  kaimu OCD  wilaya ya Kahama na  Maro Kenyunko

Jeshi la sungusungu likiwa katika picha ya pamoja  na viongozi wa jeshi la polisi 

Wanawake kata ya Mondo wakijitokeza kumsikiliza kamanda wa polisi kwenye mkutano wa hadhara kata ya Mondo wilayani Kahama.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464