KATIBU tawala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Timothy Ndanya amewashauri wataalamu wa halmashauri ya Msalala wanapofunga hesabu za mwisho wa mwaka wahakikishe hoja zote zinajibiwa vizuri ili kuondokana na hati chafu.
Ndanya ametoa ushauri huo leo tarehe 29/09/2022 alipokuwa kwenye kikao cha baraza la madiwani maalum la kufunga mwaka wa hesabu za serikali ambao ulianza Agosti 15 hadi tarehe 30 Septemba 2022 katika halmashauri ya
Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
“Mkiwa mmejibu
hoja zenu zote vizuri mna uhakika wa
kupata hati safi na sasa tumeanza robo ya kwanza ya mwaka lazima mkusanye mapato ya uhakika
kwa malengo mliojiwekea”, amesema Ndanya.
Makamu
mwenyekiti wa halmashauri hiyo Flora Sagasaga amesema kuwa watahakikisha yote yanasimamiwa vizuri ili kupata hati safi.
“Tunataka na
taasisi zingine kama Ruwasa,Tarura na Tanesco zihakikishe wanaleta taarifa zao mapema ili kuzipitia lengo la kununuliwa vishikwambi
ni kupata taarifa mapema ila tunakwenda vizuri tushikamane ili kumsaidia Rais
wetu”amesema Sagasaga.
Diwani wa kata ya Ikinda Matrida Musoma amesema kuwa wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za miradi mbalimbali nayo imesimamiwa vizuri na wataalamu.
“Taarifa hizi ambazo tumezipitia leo imeonyesha tathimini ya mwaka mzima hivyo tumeona wapi tumeteleza na tuungane kwa pamoja tusimamie vizuri zaidi”amesema diwani Musoma.