LHRC WATOA MSAADA WA KISHERIA SINGIDA MAMIA WAJITOKEZA


Wananchi wakipata msaada wa kisheria.

Wananchi wakipata msaada wa kisheria.

Wananchi wakipata msaada wa kisheria.

Wananchi wakipata msaada wa kisheria.

Mwandishi wetu

Arusha.Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu(LHRC) kimeanza kutoa bure ushauri wa kisheria kwa wananchi wa mkoa wa Singida.
 
Akizungumza na waandishi,Wakili Hamis Mayombo amesema zoezi hilo ambalo limeanza jumatatu wiki hii litakuwa la wiki moja.

Wakili Mayombo amesema hadi Sasa mashauri mengi ambayo wamekuwa wakipokea ni migogoro ya ardhu,masuala ya mirathi na utawala bora, baadhi yatafikishwa mahakamani na mengine kupatiwa suluhu.

Wakili Mayombo ambaye ni Mkuu wa LHRC Ofisi ya Arusha,alisema mashauri ya ndoa yanatokana na migogoro ya kifamilia huku migogoro ya ardhi ikitokana na uvamizi wa ardhi.

Wakili w Fides Mwenda alisema baadhi ya mashauri ambayo wamepokea tayari yamefikishwa mahakamani na mengine bado.

"lakini pia kuna malalamiko ya viongozi kukiuka misingi ya utawala bora hivyo wamelalamikiwa"amesema.

Mmoja wa Wananchi hao, Michael Itembe alisema anataka msaada wa kisheria kusaidiwa kupata shamba lake ambalo limevamiwa na ndugu zake na kulima bila idhini yake.

"naomba LHRC isaidie kisitishwa kilimwa katika ardhi yangu hadi kesi ya msingi imalizike"amesema.

LHRC itatoa huduma za kisheria kwa wiki moja mkoani Singida.

Jumanne Issa alieleza kuvamia ardhi yake na tayari shauri limefishwa mahakama I lakini hata hivyo bado suluhu haijapatikana.

Rehema Peter mkazi wilaya ya Ikungi alieleza kusumbuliwa na ndugu wa marehemu mume wake katika suala la mirathi kwani wanataka kunyang'a ya Mali zake.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464