Na Kareny
Masasy, Kahama
DAKTARI bingwa wa magonjwa ya watoto kutoka hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga dk Mwita Ngutunyi amesema kuwa mila na desturi za kumuachisha mtoto maziwa ya mama pale anapokuwa mama mjamzito kwa madai yataleta madhara inawatesa watoto.
Dk Ngutunyi
ameyasema hayo jana katika mada ya hali ya lishe na huduma kwa
watoto alipokuwa kwenye mafunzo ya
wataalamu wa afya, maafisa lishe na ustawi wa jamii kutoka kanda ya ziwa iliyojumuisha mikoa mitano
ya Mara,Mwanza,Simiyu Geita na Shinyanga
“Mila ya
kumuachisha mtoto akiwa na miezi kadhaa wakati mama akiwa mjamzito ni
hatari inasumbua hivyo wazazi wanaweza kutumia mbinu ya uzazi
wa mpango kupangilia ili watoto wao waendelee kuwa na afya nzuri na mzazi arudishe afya yake”amesema Ngutunyi..
Dkt Ngutunyi
alisema kuwa wazazi wasipotumia uzazi wa
mpango mtoto hata ukuaji wake unakuwa
sio mzuri na kumrudisha mtoto kukaa kwenye hali yake huwa ni ngumu na gharama ni kubwa hivyo
ujauzito unatakiwa upatikane kwa mpango.
Dk Ngutunyi
amesema kuwa lengo la mafunzo ni
kuainisha vitu vinavyosababisha utapiamlo
ambao wakuzidisha chakula haupo sana kwa watoto na upo ule wa ukosefu wa lishe yenye mpangilio
unaohitajika.
“ukosefu wa
madini ya vitamin A utamfanya mtoto kuwa
na uoni hafifu au kutokuona kabisa na ukosefu wa madini chuma unachangia upungufu wa damu mwilini na
madini joto unamfanya mtoto kutokukua vizuri”amesema Ngutunyi.
Ofisa lishe
mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka amesema kuwa
asilimia 71 ya watoto chini ya umri wa miaka mitano mkoani Shinyanga wanaupungufu wa damu ikiwa baadhi ya wazazi wamekuwa hawanyonyeshi
kwa utaratibu unaotakiwa maziwa ya mama ambayo yana virutubishi vingi.
Baadhi ya
maafisa lishe Bundi Clemet na Peter
Shimba wamesema kuwa mama akiwa mjamzito anapaswa
kunyonyesha kwa kipindi cha umri wa mimba
yake ikifika miezi saba hakuna madhara na wengi huwakatisha hasa
wakiwa na ujauzito nakuwatenga.