MGODI WA MWADUI WAFANIKIWA KUKARABATI GARI LA ZIMAMOTO SHINYANGA

 
    Gari la Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga ambalo limefanyiwa matengenezo na Mgodi wa almasi wa Kampuni ya Williamson Diamond baada ya kupata ajali likiwa kwenye majaribio.

                      SUZY LUHENDE Shinyanga Press Club Blog 

Mgodi wa Almasi wa Kampuni ya Williamson Diamond umekamilisha matengenezo ya gari la Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga ambalo lilipata ajali wakati wa majaribio Februari mwaka huu na kuharibika vibaya .

Akikabidhi gari hilo kwa Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga baada ya kulifanyia matengenezo,  Mwakilishi wa Meneja Mkuu wa Mgodi ambaye pia ni meneja mahusiano ya jamii Bernard Mihayo,amesema wameamuwa kusaidia matengenezo ya gari la Jeshi la zimamoto ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa urahisi pindi yanapotokea majanga. 

Mihayo amesema gari hilo ni msaada mkubwa kwa jamii kuokoa maisha ya watu na mali zao yanapotokea majanga ya moto  litasaidia uokoaji kwa wakati kutokana na kuwa na vifaa  vyote vinavyohitajika na kuondoa changamoto iliyokuwa ikijitokeza awali ambapo gharama za matengenezo ni zaidi ya milioni 21.

“Tulipokea ombi la Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga George Mrutu Juni mosi mwaka huu kuomba msaada wa matengenezo ya gari hili,ombi lake tulilipokea na kuanza kufanya maandalizi ya matengenezo tunashukuru tumekamilisha na leo hii tuna likabidhi ili likafanye kazi”amesema Mihayo. 

Kwa upande wake  mhandisi mkuu wa kampuni ya Williamson Diamonds  Shagembe Mipawa amesema wanafanya kazi kwa kushirikiana na serikali kwa jambo lolote kwa kuwa wao pia ni sehemu ya jamii na kutenga muda wa kufanya shughuli zao na kusaidia jamii. 

 Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga George Mrutu amesema anaishukuru kampuni hiyo na jopo lote la mafundi,  kwa kukubali ombi lao na kufanya matengenezo kwa wakati baada ya gari hilo kupata ajali ya barabarani na kupinduka likiwa katika majaribio.

 Mwakilishi wa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond ambaye pia ni Meneja mahusiano ya jamii Bernard Mihayo akimkabidhi gari Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga George Mrutu.
Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga George Mrutu akitoa shukrani kwa uongozi wa mgodi.
Mwakilishi wa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond ambaye pia ni Meneja mahusiano ya jamii Bernard Mihayo akizungumza wakati wa kukabidhi gari la zimamoto
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa almasi Kampuni ya Williamson Diamond Shagembe Mipawa anaeleza namna ambavyo wameweza kutengeneza gari hilo.
  Fundi wa Gereji ya mgodi  Saidi Salum aliyehusika katika matengenezo ya gari akisaidiana na jopo lake la mafundi.
  Baadhi ya askari wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464