Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifungua kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ameonya upotoshaji dhidi ya chanjo ya Polio ambayo inatolewa kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano.
Mjema akizungumza leo Septemba 2, 2022 kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi June 2022, pamoja na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Amewataka viongozi wa Mkoa huo pamoja na Wataalam kuhamasisha wananchi kuwapatia watoto wa chanjo hiyo ya Polio ambayo inatolewa kwa njia ya Matone, pamoja na kukanusha upotoshaji wowote ule dhidi ya chanjo hiyo ya Polio.
“Chanjo hizi ni salama na zimethibitishwa na Wizara ya afya pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), hivyo niwaombe viongozi na wataalamu muendelee kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa watoto kupata Chanjo ya Polio kupitia majukwa mbalimbali,”amesema Mjema.
“Tusipochanja watoto wetu chanjo hii ya Polio, tutapata watoto wenye ulemavu na wasio na Afya, na Taifa letu hapo baadae litakuja kukosa wataalam wakiwamo Madaktari, hivyo tuhakikishe tunafikia malengo na kukanusha upotoshaji wowote dhidi ya chanjo hii ya Polio,”ameongeza.
Aidha, akizungumzia utoaji wa chanjo ya UVIKO-19, amesema katika mkoa huo hadi kufikia Agosti 31 mwaka huu, jumla ya watu 735,844 wamepata chanjo hiyo sawa na asilimia 73, na kuufanya mkoa huo kushika nafasi ya tano kitaifa.
Katika hatua nyingine Mjema ameziagiza Halmashauri zote mkoani humo kuendelea kutoa fedha za afua za Lishe Shilingi 1000 kila mwezi kwa kila mtoto aliyechini ya umri wa miaka mitano pamoja na kufanya vikao vya tathmini ya lishe ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe.
Kwa upande wake Mratibu wa chanjo mkoani Shinyanga Timothy Sosoma, amesema dozi walizopokea za chanjo ya Polio awamu hii ya tatu ni 492,000 na wanatarajia kufikia watoto 445,681 na hadi kufikia jana wameshatoa chanjo hiyo kwa watoto 35,885.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifungua kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akizungumza kwenye kikao hicho.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk, Yudas Ndugile akizungumza kwenye kikao hicho.
Mratibu wa chanjo Mkoa wa Shinyanga Timothy Sosoma akiwasilisha taarifa za chanjo kwenye kikao hicho.
Mratibu wa Lishe Mkoa wa Shinyanga Denis Madeleke akiwasilisha taarifa za Lishe kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.