RC MJEMA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA UJENZI MIUNDOMBINU YA BARABARA, AONYA KUTEKELEZWA CHINI YA KIWANGO

 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza kwenye utiaji saini mikataba ujenzi miundombinu ya barabara mkoani humo, Kati ya TARURA na Wakandarasi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amewataka Wakandarasi ambao wamesaini mikataba ya ujenzi wa miundombinu ya barabara mkoani humo kuitekeleza kwa ubora unaotakiwa pamoja na kuikamilisha kwa wakati.

Mjema amebainisha hayo leo Septemba 6, 2022 wakati akishuhudia utiaji saini mikataba 15 ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja na makaravati mkoani humo, kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi, yenye thamani ya Sh.bilioni 2.6.

Amesema hawatakubali wala kupokea barabara ambayo itajengwa chini ya kiwango, na kuwataka Wakandarasi hao waifanye kazi yao kwa weledi mkubwa na kwa viwango vinavyotakiwa.

“Hatutakubali wala kupokea ujenzi wa barabara ambayo ipo chini ya kiwango,”amesema Mjema.

“Fedha zipo na tunataka barabara hizi zidumu ndani ya miaka 20 na siyo mwaka mmoja tu barabara inakuwa mbovu hilo hatutaki, bali fanyeni kazi zenu kwa ufanisi mkubwa na mshindane na Wakandarasi kutoka Nje ya nchi,”ameongeza.

Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amesema miundombinu ya barabara ni kiungo muhimu cha ukuaji wa uchumi na kuwasihi Wakandarasi waitekeleze miradi hiyo kwa ubora zaidi.

Kwa upande wake Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoani Shinyanga Mhandisi Oscar Mlekwa, amesema wametia saini Mikataba 15 na Wakandarasi ambao ni Wazawa, kwa ajili ya kujenga miundombinu ya barabara, madaraja na makaravati mkoani humo.

Amesema Mikataba ya ujenzi wa miundombinu hiyo ya barabara mkoani humo kwa kiwango cha Changalawe ni wa miezi sita, huku akibainisha pia katika mwaka wa fedha (2022/ 2023) wametengewa pia kiasi cha fedha Sh.bilioni 15 kwa ajili ya matengezo ya barabara mkoani humo.

Nao baadhi ya Wakandarasi akiwamo Flora Gabba, wameipongeza Serikali kwa kujali Wakandarasi ambao ni wazawa na kuwapatia kazi, huku wakiahidi kutowa angusha na kutekeleza kazi zao kwa kiwango bora na kuikamilisha kwa wakati ndani muda uliopangwa.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza kwenye utiaji saini mikataba ujenzi miundombinu ya barabara mkoani humo, Kati ya TARURA na Wakandarasi.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye utiaji saini mikataba ujenzi miundombinu ya barabara mkoani humo, Kati ya TARURA na Wakandarasi.

Meneja wa TARURA mkoani Shinyanga Mhandisi Oscar Mlekwa, akizungumza kwenye utiaji saini mikataba ujenzi miundombinu ya barabara mkoani humo, Kati ya TARURA na Wakandarasi.

Meneja wa TARURA mkoani Shinyanga (kulia) akikabidhiana Mkataba wa ujenzi wa barabara mara baada ya kumaliza kutia saini na Mkurugenzi wa Kampuni ya ujenzi ya Mida Women Group Milka Marisham.

Meneja wa TARURA mkoani Shinyanga (kulia) akikabidhiana Mkataba wa ujenzi wa barabara mara baada ya kumaliza kutia saini na Mkurugenzi wa Kampuni ya ujenzi ya Corsyne Consult LTD Denis Kasoka.
Meneja wa TARURA mkoani Shinyanga (kulia) akikabidhiana Mkataba wa ujenzi wa barabara mara baada ya kumaliza kutia saini na Mkurugenzi wa Kampuni ya ujenzi ya Joline Women Group Flora Gabba.

Kikao cha ushuhudiaji utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja na makaravati kikiendelea.

Kikao cha ushuhudiaji utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja na makaravati kikiendelea.

Kikao cha ushuhudiaji utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja na makaravati kikiendelea.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464