SHINYANGA WAZINDUA VITABU VYA MIKAKATI YA KUBORESHA ELIMU NCHINI, RC MJEMA AWASIHI WAZAZI KUFUATILIA MAENDELEO YA ELIMU YA WATOTO WAO


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akiwa ameshika vitabu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini (kulia) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo.

Na Halima Khoya, SHINYANGA

SERIKALI mkoani Shinyanga, imezindua Rasmi vitabu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini.

Vitabu hivyo vimezinduliwa leo Septemba 6, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu.

Mjema akizungumza wakati wa uzinduzi wa vitabu hivyo, amewataka wadau wote kushirikiana katika uboreshaji wa elimu, wakiwamo na wazazi kufuatilia maendeleo ya elimu ya watoto wao na siyo kuwatelekezea walimu.

“Vitabu hivi vya mikakati ya kuboresha elimu nchini vitasaidia kubaini changamoto za elimu, na kuweka mikakati ya kuzitafutia ufumbuzi,”amesema Mjema.

“Katika kuboresha ubora wa elimu, walimu naombeni muwe mnakaa vikao na wazazi , pamoja na wazazi mtekeleze majukumu kwa watoto wenu na kufuatilia maendeleo yao ya elimu,” ameongeza.

Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ametoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuboresha Sekta ya elimu na kujenga miundo mbinu rafiki kwa wanafunzi.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa Shinyanga Dafroza Ndalichako, amesema kumekuwa na changamoto katika uendeshaji elimu ya Msingi na Sekondari, ambapo vitabu hivyo ndiyo suluhisho na kuboresha elimu hapa nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye kikao cha uzinduzi vitabu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini mkoani humo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Siza Tumbo, akizungumza kwenye kikao cha uzinduzi vitabu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini mkoani humo.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye kikao cha uzinduzi vitabu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini mkoani humo.

Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako, akizungumza kwenye kikao cha uzinduzi vitabu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini mkoani humo.

Wadau wa elimu wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Vitabu vya Mikakati ya kuboresha elimu nchini mkoani Shinyanga.

Wadau wa elimu wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Vitabu vya Mikakati ya kuboresha elimu nchini mkoani Shinyanga.

Wadau wa elimu wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Vitabu vya Mikakati ya kuboresha elimu nchini mkoani Shinyanga. 
PICHA NA MARCO MADUHU.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464