Mwezeshaji kwenye mafunzo ya utoaji huduma kwa watoto waliopatwa na utapiamlo ambaye ni Ofisa lishe mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka.
Mafunzo hayo
yamefanyika leo tarehe 19/09/2022 mjini Kahama mkoani Shinyanga nakuratibiwa na wizara ya
afya ambapo mikoa ya Mwanza,Geita,Simiyu,Mara na Shinyanga imeshiriki.
Mwezeshaji wa matibabu ya utapiamlo
kitaifa Getrud Mollel amesema kuwa jamii inatakiwa iwekeze
kwenye umri mdogo wa watoto wao ili kuondokana na taifa tegemezi.
Mollel amesema
kuwa wazazi lazima wawajali watoto kwa lishe
bora wenye mpangilio ili kuwaepusha na utapiamlo
na kuwe na taifa imara kwa miaka ijayo kwa
kuwa na watoto wenye uelewa mzuri wawapo
darasani na kwenye mazingira yanayowazunguka wakuweza kujitegemea bila
utegemezi.
Ofisa lishe
mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka ambaye alikuwa mwezeshaji katika mafunzo hayo amesema hapa nchini ni asilimia 53 ya vifo vya watoto chini ya
umri wa miaka mitano vimetokea vikisababishwa na utapiamlo hivyo elimu itolewe kwa wazazi.
Madeleka amewataka
maafisa lishe kanda ya ziwa kutoa
takwimu zinazoendana na uhalisia wa maeneo yao ambapo alieleza kanda ya ziwa bado kuna
udumavu kwa watoto ikiwemo mkoa wa Shinyanga una asilimia 32 na Simiyu ni asilimia 31.
“Kwa mujibu
wa utafiti wa kitaifa wa hali ya lishe uliotolewa na Tanzania National Nutrition suvey (TNNS) mwaka
2018 umebainisha kuwa ni asilimia 31.8 ya
watoto chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa
na asilimia 3.5 wanautapia mlo mkali” amesema Madeleka.
Bundi Clementi
ofisa lishe kutoka halmashauri ya Musoma
amesema kuwa wameshukuru kwa kuandaa mafunzo haya kwani wamejifunza kuhudumia
watoto wenye utapiamlo mkali na vitu vya
kufanyia kazi kitaalamu.
“Mtoto akiwa
na utapiamlo mkali lazima alazwe hata kama hana changamoto zingine za
kiafya,akiwa mkodefu lazima uangalie historia alikotokea kwenye jamii
nakushirikisha maafisa wa ustawi wa jamii huenda pia mazingira anayoishi ndiyo yamemfanya hivyo" amesema Clement.
Dkt James Wankuru kutoka halmashauri ya mji Bunda amesema kuwa
mafunzo haya ni muhimu kwao sababu takwimu zimetolewa nakuelezwa kuwa watoto
Millioni tatu wana utapiamlo hapa nchini.
Dkt Wankuru amesema kuwa mfumo wa utoaji matibabu kwa watoto wenye utapiamlo umebadilika mojawapo utolewaji wa matone ya Vitamini A watayatoa kwa wale wenye dalili za utapiamlo na siyo walio nao tayari kama ilivyokuwa zamani.
Mwezeshaji kwenye mafunzo ya utoaji huduma kwa watoto waliopatwa na utapiamlo ambaye ni Ofisa lishe mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka
Watlaaamu wa afya,ustawi wa jamii na maafisa lishe kutoka mikoa mitano ya kanda ya ziwa wakipatiwa mafunzo juu ya huduma kwa watoto waliopata utapiamlo na wenye dalili,
Maafisa lishe wakisikiliza kwa umakini mada zilizokuwa zikitolewa.
Mwezeshaji kwenye mafunzo ya utoaji huduma kwa watoto waliopatwa na utapiamlo ambaye ni Ofisa lishe mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka
Mwezeshaji wa wa matibabu ya utapiamlo kitaifa Getrud Mollel.