WATOTO KUFUNDISHWA KOMPUTA KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI HALIKWEPEKI



Wahitimu wa darasa la saba mwaka 2022 wa shule ya msingi Citizen , wakiimba nyimbo yao ya kuwaaga wenzao katika mahafali ya tatu.

Na Patrick Mabula, KAHAMA

MWALIMU wa chuo cha walimu mkoani Shinyanga , Peter Malimi amesema suala la kufundisha watoto kwa kutumia kompyuta katika shule zetu za sekondari na msingi halikwepeki na kuzitaka kujipanga ili watoto waweze kufundishwa elimu hiyo.

Malimi ametoa wito huo alipokuwa akiongea kwa niaba ya mkuu wa chuo cha walimu kilichopo mkoani Shinyanga katika mahafali ya tatu ya darasa la saba na chekechea ya shule ya msingi Citizen iliyopo mjini Ushirombo na kuzitaka shule kuweka mazingira ya kuwafundisha watoto kwa kompyuta.

Amesema suala la kufundisha watoto kwa kutumia teknolojia ya ya kompyuta kwa kipindi hiki halikwepeki na ambako alizitaka shule zetu kuhakikisha zinaweka mazingira ya kufundisha somo hilo la kidigitali.

Malimi amesema katika shule zetu kwa sasa walimu wanapaswa kuandaa mazingira kwa baadhi ya vyumba vya madarasa kuweza kufundisha kwa kutumia kompyuta likiwemo somo la Tehama kwa vitendo katika dunia hii ya kidigitali na kuipongeza shule ya Citizeni kwa kuanza kufundisha kwa mfumo huo.

Mkuu wa shule hiyo Rodgers Mgimbwa amesema wameendelea kuboresha mazingira ili kuwawezesha watoto kusoma vizuri pamoja na kutenga chumba maalumu cha kuwafundisha somo la Tehama katika dunia ya sasa ya kidigitali na kuwaalika wazazi za walezi kupelaka watoto wao hapo na kuwaomba kulipa ada kwa wakati.

Mkurugenzi wa shule ya Citizen Silvano Lujengi amesema tayari shule yake ina kompyuta 10 na sehemu ya maalumu katika jengo la utawala ambapo watoto wataweza kufundishwa kwa njia hiyo.

Lujengi amesema shule yake inataendelea kutatua changamoto mbalimbali zilizopo pamoja na kuboresha mazingira ya watoto kusoma vizuri waweze kufanya vizuri kitaaluma ambapo mwaka juzi waliweza kuongoza kitaifa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa taifa wa kumaliza darasa la saba.

Afisa elimu wa kata ya Igulwa Peter Malegesi akiongea kwa niaba ya afisa elimu wa shule ya msingi wa wilaya ya Bukombe alipongeza shule ya Citizen ambayo imekuwa chahu wilayani kwa watoto kufanya vizuri kitaaluma pamoja na ufaulu mzuri kwa mtihani wa taifa wa kuhitimu darasa la saba.








Mkurugenzi wa shule ya msingi Citizen ,Silvano Lujegi wa kushoto akiwa na mkuu wa shule hiyo Rodgers Mgimbwa katika mahafali ya tatu ya wahitimu wa darasa la saba shuleni hapo.

Wahitimu wa darasa la saba mwaka 2022 wa shule ya msingi Citizen , wakiimba nyimbo yao ya kuwaaga wenzao katika mahafali ya tatu.

Mkurugenzi wa shule ya msingi Citizen , Silvano Lujegi akitoa hotuba yake kwenye mahafa ya tatu ya wahitimu wa darasa la saba mwaka huu 2022 .





Mgeni rasmi katika mahafali ya tatu ya darasa la saba ya shule ya msingi Citizen , ambae mwalimu wa chuo cha walimu mkoani Shinyanga ,Peter Malimu alipokuwa akiongea kwa niaba ya mkuu wa chuo cha walimu Shinyanaga aliyekuwa amemwakilisha.





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464