Mwenyekiti wa Klabu ya Mazingira Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Mariam Enock (wa kwanza kushoto) akitoa elimu ya unawaji mikono kwa wanafunzi wenzake shuleni hapo.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
SHIRIKA la Maendeleo la Uholanzi (SNV),limeadhimisha siku ya unawaji mikono duniani katika Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga kwa kutoa elimu ya unawaji mikono sahihi kwa wanafunzi ili kuwaepusha na maradhi mbalimbali.
Afisa Msaidizi wa Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini (WASH SDG) kutoka SNV Issack Msumba, akizungumza shuleni hapo, amesema siku ya unawaji mikono duniani huadhimishwa kila mwaka Oktoba 15, lakini wao wameadhimisha leo Oktoba 18, 2022, kutokana na siku hiyo kuangukia Jumamosi ambayo wanafunzi walikuwa majumbani mwao.
Amesema wamefanya maadhimisho hayo katika shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule walizozipatia mafunzo ya usafi wa mazingira pamoja na kuunda klabu ya Mazingira, ambapo wanafunzi kupitia klabu yao hufundishana wao kwa wao namna ya kuzingatia usafi kwa kunawa mikono.
“Wanafunzi wakielewa zaidi namna ya unawaji mikono kwa usahihi, wataisambaza elimu hii majumbani mwao na kuwa mabalozi wazuri,” amesema Msumba.
Naye Afisa elimu masuala ya Afya katika Shule za Sekondari na Msingi Manispaa ya Shinyanga Beatrice Mbonea, akizungumza katika maadhimisho hayo, amewataka wanafunzi wazingatie usafi muda wote kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka ili kuepuka kula uchafu kujiepusha na maradhi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Mazingira shuleni hapo Mariam Enock, amesema elimu hiyo ya usafi wa mazingira imewasaidia wanafunzi kuzingatia usafi muda wote, kwa kunawa mikono mara kwa mara, na kuwaepusha na maradhi mbalimbali yatokanayo na uchafu.
Afisa Msaidizi wa Mradi wa usafi wa mazingira mijini (WASH SDG) kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) Izack Msumba akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya unawaji mikono duniani katika Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Martine Mponda akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya unawaji mikono.
Naye Afisa elimu masuala ya Afya katika Shule za Sekondari na Msingi Manispaa ya Shinyanga Beatrice Mbonea akizungumza katika maadhimisho hayo ya siku ya unawaji mikono katika shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Mwalimu wa Mazingira Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Ernest Ngarama akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya unawaji mikono shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Mazingira Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Mariam Enock, akizungumza kwenye maadhimisho ya unawaji mikono duniani shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Mazingira Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Mariamu Enock, akitoa elimu ya unawaji mikono kwa usahihi kwa wanafunzi wenzake, mafunzo ambayo awali walishapewa na SNV kupitia klabu yao.
Mfunzo ya unawaji mikono kwa usahihi yakiendelea kutolewa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ili kujikinga na maradhi mbalimbali hasa wanapotoka chooni kujisaidia.
Mafunzo ya unawaji mikono kwa usahihi yakiendelea kutolewa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ili kujikinga na maradhi mbalimbali hasa wanapotoka chooni kujisaidia.
Mfunzo ya unawaji mikono kwa usahihi yakiendelea kutolewa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ili kujikinga na maradhi mbalimbali hasa wanapotoka chooni kujisaidia.
Walimu wa shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakinawa mikono kwenye maadhimisho hayo ya siku ya unawaji mikono duniani.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya unawaji mikono duniani shuleni hapo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya unawaji mikono duniani shuleni hapo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya unawaji mikono duniani shuleni hapo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya unawaji mikono duniani shuleni hapo.