MANISPAA YA SHINYANGA YAJAYO YANAFURAHISHA, WAFANYABIASHARA WAHIMIZWA KULIPA MAPATO YA SERIKALI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye kikao cha wadau wa maendeleo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga, imewasilisha taarifa ya uelekeo wa Manispaa hiyo kimaendeleo na ukuaji kiuchumi ifikapo mwaka 2025.

Taarifa hiyo imewasilishwa leo Oktoba 7, 2022 kwenye kikao kazi cha wadau wa Maendeleo Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo.

Akiwasilisha taarifa hiyo Kaimu Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Fidelis Kabuje, amesema Manispaa ya Shinyanga imejiwekea mikakati yake ya kimaendeleo na kukuza uchumi, na ifikapo mwaka 2025 itakuwa imepiga hatua kubwa.

Amesema dira ya Manispaa hiyo hadi ifikapo mwaka huo 2025, ni kuwa na mji salama pamoja kuwepo na fursa nyingi za uwekezaji kiuchumi vikiwamo viwanda, sambamba na kuongeza pato la mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Vipaumbele vya halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuanzia sasa hadi ndani ya miaka mitano kwa kufuata dira ya maendeleo ya taifa, ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii, ustawi wa maisha ya wananchi, kukuza uchumi wa wananchi.,

“Kuimarisha utawala bora, na ugawaji wa rasilimali kwenye miradi kielelezo kwa ajili ya maendeleo ya viwanda, kupima na kumilikisha ardhi kwa wananchi, pamoja na kupanda Miti milioni 1.5 kila mwaka”amesema Kabuje.

Aidha, ameitaja miradi mikakati ambayo itatekelezwa ndani ya miaka hiyo mitano, kuwa ni ujenzi wa Shoping Mall, ukumbi wa wazi, Soko la kisasa, maegesho ya Malori, viwanda vidogo, Stendi mpya ya mabasi, kuendeleza eneo la Tanganyika Packers.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, amesema kwa mikakati ambayo wamejiwekea ni kutaka Manispaa hiyo iwe kitovu cha fursa za biashara sababu ndiyo makao makuu ya mkoa.

Amesema ufinyu wa fursa katika Manispaa ya Shinyanga ndiyo sababu imekuwa ikishindwa kukua kimaendeleo, sababu ya watu kwenda kutafuta fursa maeneo ya pembezoni, ambapo malengo yake yeye ni kutaka fursa zipatikane hapo hapo Shinyanga, na wananchi hakuna tena kufauta bidhaa wilayani Kahama, wala Jijini Mwanza.

“Tunataka Mji wa Shinyanga tuubadilishe uwe wa kibiashara, sababu asilimia 85 ya wananchi wake wanafanya shughuli za kilimo, na asilimia 15 ndiyo wanafanya biashara, ndiyo sababu mji unashindwa kukua kwa kasi na kwenda taratibu,”anasema Satura,

“Sasa hivi tumeanza na kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwamo ya ujenzi wa Masoko, Stendi, huduma za afya, barabara na pia tumeanza mchakato wa vyuo vya hapa Shinyanga kuvipandisha hadhi ili viwe vyuo vikuu na kuongeza idadi ya watu, na mji uwe na muingiliano wa kibiashara,”ameongeza.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amesema ili Shinyanga ipate kukua kwa kasi kimaendeleo, ni pamoja na ulipaji wa mapato ikiwamo tozo ya ushuru wa huduma (Service Levy) ambacho ndiyo chanzo kikubwa cha mapato ya Manispaa hiyo, fedha ambazo zitatekeleza mipango yote hiyo na kuifanya Shinyanga kuwa jiji.

Amesema mapato ya ndani ndiyo chanzo kikubwa cha maendeleo, na kuwasihi wafanyabiashara waendelee kulipa mapato hayo kama wanavyofanya hivi sasa, ili Serikali ipate pesa na kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo na kuwaboreshea miundombinu na kufanya bishara zao katika mazingira Rafiki.

“Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika mwaka wa fedha (2021-2022) tumekusanya mapato ya ndani Sh.bilioni 5.06 sawa na asilimia 125 na kuongoza kitaifa, na tozo ya ushuru wa huduma tumekusanya Sh.milioni 800 na hiki ndicho chanzo chetu kikubwa cha mapato,”amesema Masumbuko

Pia ameipongeza Kamati ya ukusanyaji mapato ya Manispaa hiyo ambayo iliundwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kuwa imekuwa kichocheo kikubwa cha Manispaa hiyo kupaa kwenye ukusanyaji wa mapato, ambapo tangu ianze kazi ndani ya miezi mitatu tu zimekusanywa Sh.milioni 451.2

Aidha, Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, akizungumza kwenye kikao hicho ,amesema kwa mikakati hiyo ndani ya miaka mitano anaiona Shinyanga Mpya.

Nao wadau mbalimbali wa maendeleo wakichangia mjadala kwenye kikao hicho, wamepongeza kushirikishwa kwenye mikakati hiyo ya kuikuza kimaendeleo na kiuchumi manispaa ya Shinyanga, na kuahidi kushirikiana kwa kila hatua ili mipango hiyo ifanikiwe na kuubadilisha mji wa Shinyanga.

Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akizungumza kwenye kikao hicho.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye kikao hicho.

Katibu wa Kamati ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dk. Kulwa Meshack akizungumza kwenye kikao hicho.

Kaimu Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Fidelis Kabuje,akiwasilisha taarifa ya uelekeo wa Manispaa ya Shinyanga kimaendeleo na kiuchumi ifikapo mwaka 2025.

Afisa Maendeleo ya Jamii John Tesha akiwasilisha taarifa ya ukusanyaji mapato ya ndani ya Tozo ya huduma ambayo yalichangizwa na Kamati ya ukusanyaji mapato ya ndani ya halmashauri ya Manispaa hiyo.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464