Na Kareny Masasy, Msalala
MKUU wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Festo Kiswaga amezitaka halmashauri kuhakikisha zinatoa sh 1,000 zilizotengwa kwa ajili ya watoto kwenye masuala ya lishe na kutoona alama nyekundu ikimaanisha kufanya vibaya kwenye kadi..
Kiswaga
amesema hayo leo tarehe 17/010/2022 alipokuwa akikabidhi pikipiki kwa afisa lishe, afisa afya na mratibu wa huduma ngazi ya jamii katika halmashauri ya Msalala zilizotolewa na
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu alipokuwa akisaini mkataba wa lishe.
Kiswaga
amesema pikipiki hizo wazitumie kufanya
kazi kwa bidii kama ilivyoagizwa na Rais
Samia Suluhu ambapo mkataba huo
naye alisainishwa kutoka kwa mkuu wa mkoa Sophia Mjema nakuzitaka halmashauri za Ushetu na Msalala zisiwe nyuma katika
masuala ya lishe na fedha walizozitenga zitolewe kwa wakati .
“Tumeweka
mikataba hivyo wakurugezi washuke kwa watendaji wa kata pikipiki hizi
wamepewa waweze kufuatilia ziwanufaishe wananchi na sh 1000 zinazokatwa kwaajili ya watoto kuhusu
lishe zifike kwa wakati kulikuwepo na ucheleweshwaji”amesema Kiswaga.
Kiswaga amesema hataki kupata alama nyekundu kwenye kadi katika wilaya yake kwenye halmashauri zote akikuta hivyo muhusika ajiandae kuacha kazi huo utakuwa ni uzembe maana kitendea kazi unacho mafuta na ukarabati vyote vinawezeshwa na serikali.
Kaimu ofisa
Lishe halmashauri ya Msalala Peter
Shimba amesema wametenga zaidi ya
sh Millioni 61.5 mapato ya ndani kwaajili ya lishe kwa watoto katika
bajeti ya mwaka 2022/2023.
Shimba
amesema viashiria vya ukosefu wa lishe huvitazama kwa mjamzito sababu ndiye amebeba mtoto
nakumtegemea katika ukuaji wake.
Shimba amesema miezi ya kuzingati ulaji mzuri kwa mtoto ni kuanzia umri wa
miezi 0 hadi 23 akikosa hapo mtoto akipata udumavu ni vigumu kumrekebisha na kurudi kwenye hali
nzuri.
Shimba amesema watoto kwa mwaka jana
waliozaliwa na uzito wa chini ya kg 2.5 ni 57 sawa na asilimia 0.1.
“Halmashauri
ya Msalala ina Upungufu wa damu kwa wajawazito asilimia 4.2, ambapo kiwango cha udumavu kwa mkoa ni
asilimia 32 ukondefu asilimia 4 na uzito pungufu ni asilimia 15"amesema Shimba.
Shimba amesema kazi ya afisa lishe ni
kushughulikia mjamzito anapata lishe bora
wakati wote katika siku 1000 tangu
anapopata ujauzito na mtoto kunyonyeshwa
maziwa ya mama hadi miaka miwili
mfululizo.
Ofisa afya halmashauri ya Msalala Marthad Khojama amesema kupata usafiri atahakikisha wajawazito na watoto wanatembelewa kwenye maeneo yao kwa urahisi kwaajili ya kuhamasisha ulaji wa lishe bora katika hali ya usafi ,uwepo wa madini joto na utumiaji wa vyoo bora.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464