Wajumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Shinyanga na wajumbe wa kata ya Chamaguha wakiwa katika jengo la shule ya wazazi kata ya Chamaguha
Suzy Luhende,Shinyanga Blog
Jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini mkoani hapa imefanya ziara ya kuwaonyesha wajumbe wa kamati ya utekelezaji miradi mbalimbali za jumuia zilizomo wilayani humo, ambazo ni viwanja, na majengo ya shule.
Ziara hiyo imefanyika leo wilayani humo ambapo kamati hiyo imekagua jengo la shule ya awali iiyoko kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga, ambapo itaendelea kukagua katika kata ya Ibadakuli, Ndala na Ndembezi na Chibe ambako tayari kuna viwanja vya jumuia hiyo.
Katibu wa jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga Doris Kibabi amesema
Kamati ya utekelezaji wazazi inazidi kuhamasisha kata zingine ambazo bado hazina miradi ya aina yeyote ianzishe, ili kuhakikisha kila kata inakuwa na miradi ya kujiongezea kipato.
"Tunawahamasisha kata ya Chibe, Kolandoto, Ibadakuli, Mwamalili, Kizumbi na Mwawaza kuomba mashamba ili waanzishe kilimo cha alzeti na upandaji wa miti, ili kuweka mazingira safi, kujipatia kipato cha jumuia" amesema Kibabi.
Kibabi amesema kamati itasimamia ipasavyo kukarabati majengo na pia wanakaribishwa wawekezaji kwa ajili ya kuanzisha shule ya awali mpaka sekondari katika eneo lililopo kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga ambalo lina heka tisa (9).
"Tunawaomba wawekezaji waje kuwekeza katikae eneo la kata ya Chamaguha, kwani ni eneo kubwa ambalo linauwezo wa kujenga shule ya awali msingi, sekondari zahanati na kuweka miradi mbalimbali"amesema Kibabi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini Fue Mrindoko amesema mambo ya makundi hayana nafasi tena katika jumuia yake kinachotakiwa ni kuendelea kupambana ili kuhakikisha wanafanya maendeleo .
"Mimi na kamati yangu tutahakikisha tunafanya kazi kwa bidii zote ilikuhakikisha kila kata ya wilaya ya Shinyanga mjini ina kuwa na miradi mbalimbali ya kujiongezea kipato, ili hata tunapokuwa na shughuli zozote za kijumuia tusihangaike, tunajipanga sawa sawa,"amesema Mlindoko.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji Chacha Richard Mseti, Zulfa Dali wamesema wanamshukuru katibu Doris Kibabi kwani ni mchapa kazi amekuja Shinyanga kwa muda mfupi amefanya kitu, amehamasisha vimepatikana viwanja katika baadhi ya kata, hivyo wanaamini wakishirikiana kwa pamoja watafanya makubwa zaidi.

Mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utekelezaji na wajumbe wa kata hiyo wakiendelea kukagua jengo hilo
Wajumbe kamati ya utekelezaji wakiendelea na majadiliano jinsi ya kufanya miradi mbalimbali
Wajumbe wakiwa katika harakati ya ukaguzi wa mipaka katika eneo hilo
Mwenyekiti Fue Mrindoko na katibu wake Doris Kibabi Wakiwa makini kukagua zaidi jengo la shule hiyo
Katibu wa jumiia ya wazazi Doris Kibabi akitoa maelekezo katika ziara ya kukagua mali za jumuia hiyo

Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga Fue Mrindoko akizungumza kwenye ziara hiyo
Mwenyekiti Fue Mrindoko akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati hiyo na kuwaomba washirikiane katika kusimamia miradi ya maendeleo ya jumuia
Kamati ya utekelezaji na viongozi wa kata hiyo kutoka jumuia ya wazazi wakiwa kwenye picha ya pamoja
Wajumbe wakikagua mipaka ya kiwanja cha kata ya Chamaguha
Mwenyekiti wa mtaa wa Chamaguha akionyesha mipaka ya kiwanja hicho
Jengo la shule ya kata ya Chamaguha ambalo linatarajiwa kukarabatiwa na kuanzishwa shule ya awali