Katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi CCM Taifa Gilibert Kalima akizungumza na viongozi wa chama cha mapinduzi na jumuia zake mkoani Shinyanga
Suzy Luhende,Shinyanga blog
Katibu mkuu wa jumuia ya wazazi CCM Taifa Gilibert Kalima amewataka viongozi wote wa Chama na jumuia zake, kuvunja makundi yaliyotokana na kampeni zote za uchaguzi wa CCM, na kuacha kuhamisha makundi kwenda uchaguzi mwingine, kwani kufanya hivyo ni hatari kubwa ndani ya Chama.
Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga, katika ofisi ya jumuia ya wazazi mkoa wa Shinyanga, ambapo amesema viongozi wote wa chama na jumuia zake wavunje makundi yaliyotokana na uchaguzi na waache kuhamisha makundi kwenda uchaguzi mwingine.
"Wito wangu mimi ni kuvunja makundi yote yaliyotokana na kampeni zote za uchaguzi wa CCM, ili tuweze kufanya vizuri zaidi kwani tumekuwa na tabia mbaya ya kuhamisha makundi kupeleka kwenye uchaguzi mwingine, tunatakiwa kuyaondoa kwa sababu yakiendelea kuwepo ni hatari kubwa ndani ya chama chetu, tunatakiwa kuwa makini sana"amesema Kalima.
"Najua Shinyanga yapo makundi lakini tufike mahali tuyavunje na tuseme sasa hapana, ili tusipotoshe wananchi wetu ambao tumechukua jukumu la kuwatetea, msichukue jukumu la kumpinga mtu"amesema Kalima.
Pia Kalima amewataka viongozi, wawe makini na watu wanaopanga safu, kwa sababu watu hao ni hatari ndani ya chama, unakuta madiwani na wabunge wanapanga safu yao kuanzia mashina, kufanya hivyo ni hatari kwa uhai wa chama, badala yake wasimame vizuri kwenye vikao vya tathimini ili waendelee kuwa na chama bora cha kuaminiwa na wananchi.
"Unakuta mtu anadiliki kupanga safu kuanzia kwenye mashina, mtu huyo ni hatari kwa chama chetu anachafua na kuharibu kabisa tunatakiwa tusemane kwenye vikao vyetu ili tuendelee kuaminiwa na wananchi wetu, ili tuendelee kushika Dola tunajua Shinyanga yapo makundi, lakini tusimame kuyaondoa hayo makundi na tusimame kwenye vikao vyetu vya halmashauri tusemane ili wananchi waendelee kutuamini "amesema Kalima.
Aidha Kalima amesema wenyeviti wa mitaa na vijiji wanatakiwa kufanya mikuno baada ya miezi mitatu, kama hawafanyi wanatakiwa kukumbushwa, pia, asipotekeleza ipasavyo majukumu yake diwani halmashauri ya kata inatakiwa kumuita na kumkumbusha, na halmashauri ya wilaya pia inatakiwa kumuita mkuu wa wilaya na mkurugenzi kuwakumbusha majukimu yao kama hawatejelezi ipasavyo.
Hata hivyo katibu mkuu wa jumuia ya wazazi CCM Taifa amewapongeza kwa kuendelea kuongeza miradi mbalimbali vikiwemo vibanda vya kufanyia biashara 84 vya chama na jumuia zake katika mkoa wa Shinyanga,kwani kufanya hivyo ni kuongeza uchumi ndani ya chama.
"Jumuia ya wazazi nawapongeza sana kwa kazi mnayoifanya tunatarajia kufanya mambo matatu ya muhimu ambayo ni maadili, mazingira na afya, hivyo tunatakiwa kuongeza nguvu ili kuondoa mmomonyoko wa maadili, sisi wazazi tujikite huko ili kuondoa mauwaji vitendo vya ukatili, na tayari tumeanzisha NGO makao makuu kwa ajili ya kuelimisha maadili"amesema Kalima
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuia ya wazazi mkoa wa Shinyanga Alhaj Salm Simba amemuomba apange ziara ya kutembelee wilaya zote za Shinyanga kwa ajili ya kutoa maelekezo mbalimbali ya kimaendeleo, pia amesema maelekezo yote aliyoyatoa watayatekeleza.
Awali katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga Donald Magesa amesema tayari CCM mkoa ina vibanda 84 vya kufanyia biashara na kuna viwanja mbalimbali kwa ajili ya kufanyia miradi, hivyo ameomba waje watu wote kutoka sehemu mbalimbali waweze kuwekeza .
Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi na jumuia zake wakimsikiliza katibu mkuu wa jumuia ya wazazi CCM Taifa
Katibu mkuu wa jumuia ya wazazi CCM Taifa akisaini baada ya kufika ofisi ya wazazi mkoa wa Shinyanga
Katibu wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akitoa taarifa za kiuchumi kwa katibu wa jumuia ya wazazi Taifa
Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi mkoa wa Shinyanga Alhaj Salm Simba akizungumza
Katibu mkuu wa jumuia ya wazazi CCM Taifa Gilibert Kalima akizungumza na viongozi wa chama cha mapinduzi na jumuia zake mkoani Shinyanga
Viongozi m mbalimbali wa chama cha mapinduzi wakimsikiliza katibu mkuu
Viongozi wa CCM wakidalimiana na katibu mkuu
Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi na jumuia zake wakiwa kwenye picha ya pamoja na katibu mkuu wa jumuia ya wazazi CCM
Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi na jumuia zake wakiwa kwenye picha ya pamoja na katibu mkuu wa jumuia ya wazazi CCM
Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi mkoa wa Shinyanga Alhaj Salm Simba akizungumza
Katibu mkuu wa jumuia ya wazazi CCM Taifa Gilibert Kalima akizungumza na viongozi wa chama cha mapinduzi na jumuia zake mkoani Shinyanga
Katibu mkuu wa jumuia ya wazazi CCM Taifa akisaini baada ya kufika ofisi ya wazazi mkoa wa Shinyanga
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464