MBUNGE WA VITIMAALUM MKOA WA SHINYANGA LUCY MAYENGA AMERATIBU MATIBABU BURE KWA WANANCHI WENYE MATATIZO YA MACHO


Mbunge Viti maalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga anawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya macho

Suzy Luhende, Shinyanga

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga amewaomba wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga, kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali za magonjwa ya macho.

Akizungumza leo na Shinyanga blog Mbunge Lucy Mayenga, amesema baada ya kuona kuna changamoto kubwa ya magonjwa ya macho kwa wananchi wa Shinyanga ameamua kuratibu kambi kubwa la madaktari bingwa wa macho kutoka hospitali za KCMC Aga Khan, Mhimbili, Hindu na Mandal ambao watatoa huduma bure ya macho.

Lucy amewaomba wananchi wote kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupatiwa vipimo mbalimbali vya macho ikiwemo saratani ya macho na mtoto wa jicho, pia madaktari hao watagawa miwani bure kwa wahitaji.

"Kambi hiyo itafanyakazi kwa siku tatu ambapo kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 16 jioni mwezi huu wa kumi, kambi hii itakuwa katika uwanja wa Shycom Shinyanga mjini, hivyo wananchi wote mnaombwa kujitokeza kwa wingi, ili kufaidika na huduma hii ya bure karibuni sana wananchi wote muweze kupatiwa huduma ya macho,"amesema Mayenga.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464