MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ASIKITISHWA NA SHULE YENYE WANAFUNZI ZAIDI YA 1000 KUTUMIA MATUNDU MANNE YA VYOO HUKU WAKICHANGIA NA WALIMU


Meya wa manispaa ya Shinyanga akizungumza kwenye baraza la madiwani

Suzy Luhende Shinyanga Blog

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko ameitaka menejimenti ya manispaa ya Shinyanga kulisimamia kikakamilifu suala la vyoo vya shule za msingi na sekondari ambazo hazina vyoo  vya kutosha.
 
Ambapo amesema kuna shule ya msingi ya kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga, ambayo inawanafunzi zaidi ya 1000,lakini ina matundu manne tu ambayo inatumiwa na wanafunzi pamoja na walimu.

Hayo ameyasema leo 27,10,2022 kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, ambapo amesema inasikitisha sana shule hiyo kuwa na wanafunzi zaidi ya 1000, lakini matundu ya vyoo manne, hivyo ni vizuri suala hilo lifanyiwe kazi kwa haraka ili watoto na walimu wapate sehemu ya kujisaidi.

"Naomba sana hili lifanyiwe kazi kwa haraka ikiwa ni pamoja na shule zingine za kata mbalimbali ambazo zina changamoto kama hizi zilizowasirishwa na madiwani, inasikitisha sana kuona walimu hawana vyoo, hivyo wanasubiriana na wanafunzi kuingia choo kimoja"amesema Masumbuko.

Pia amesema madiwani wamewasirisha changamoto mbalimbali katika kata zao likiwemo la upungufu wa walimu, amesema kweli kuna upungufu mkubwa wa walimu katika shule mbalimbali za manispaa ya Shinyanga, utakuta shule ina walimu 15 wanafundisha wanafunzi zaidi ya 900 hili ni tatizo kubwa halileti uwiano hata kidogo.

"Na hili nasisitiza kutokana na uhaba wa walimu suala hili tulifanyie kazi kwa wakati ili watoto wetu wapate elimu bora na waweze kufauru vizuri, hivyo muangalie muweze kuajili walimu wa kutosha, ambayo yatakuwa ndani ya uwezo wenu mnatakiwa kuyafanyia kazi na yale yatawasilishwa sehemu husika yawasilishwe ili watoto wetu wapate elimu bora"amesema Masumbuko.
 
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema amesema suala la changamoto ya  vyoo  ni la msingi sana hivyo watakaa na menejimenti ili waangalie bajeti yao waweze kulifanyia kazi kwa kwa haraka iwezekanavyo, pia kutokana na upungufu wa walimu pamoja na watumishi wengine wanaajiliwa na serikali kuu ila tayari  wameomba wapewe kibali na katibu mkuu ofisi ya Rais, ili wapewe kibari cha ajira mbadala kwa maana wafanyakazi waliofariki waliostaafu ili kuziba nafasi hizo wakikubaliwa watafanya hivyo.

"Changamoto zilizoibuliwa na madiwani tumeziorodhesha zote na tutazifanyia kazi tutazipatia majibu, nyingi ni miundombinu  pamoja na matundu ya vyoo tutayachukua na kuyaongelea kwenye menejimenti ili tuone tunafanyaje katika mwaka wa bajeti ya mwaka 2022/2023
Madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani

Diwani viti maalumu Zuhura Waziri akiwasilisha hoja yake kwenye baraza la madiwani
Diwani Pica Chogelo akiiwasilisha hoja kwenye kikao cha baraza la madiwani
Diwani wa kata ya Kitangili Mariamu Nyangaki akiiwasilisha hoja kwenye kikao cha baraza la madiwani
Diwani wa kata ya Mwawaza Juma Nkwabi akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani
Diwani wa kata ya Lubaga akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani


Wakuu wa idara wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani
Meya wa manispaa akiwa kulia akiwa na naibu Meya wa manispaa hiyo Ester Makune na afisa utumishi wa manispaa Getruda Gisema
Diwani wa kata ya Kambarage Hasan Mwendapole akizungumza
Afisa utumishi wa manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema akifafanua jambo
Diwani viti maalumu Shella Mshandete akifuatilia jambo kwenye kikao cha baraza la madiwani
Diwani wa kata ya Chibe John Jisandu akifuatilia jambo kwenye kikao hicho
Meya wa manispaa na Naibu Meya wa manispaa wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464