MKURUGENZI MANISPAA YA SHINYANGA AWAHIDI VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUFANYA MAKUBWA KATIKA MAENDELEO
Askofu wa kanisa la IEAGT David Mabushi akimkabidhi cheti cha pongezi mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura
Suzy Luhende, Shinyanga blog
Kanisa la International Evangelical Assemblies of God Tanzania (IEAGT) limetoa cheti cha pongezi kwa mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura na kwa watumishi wote wa manispaa hiyo kwa hatua za maendeleo yanayofanyika katika mansipaa hiyo.
Akitoa vyeti hivyo vya pongezi Askofu David Mabushi leo ijumaa 21,2022 kwa niaba ya kanisa amesema dhumuni la kutoa cheti kwa kanisa ni kumpongeza mkurugenzi na watumishi wote wanaoshirikiana nae katika kufanya maendeleo mbalimbali manispaa ya Shinyanga.
"Tumejionea wenyewe maendeleo yanayofanyika katika manispaa yetu, hivyo tumeona tutoe vyeti vya pongezi kwa mkurugenzi huyu anayesimamia maendeleo haya,na kwa watumishi wanaoshirikiana nae, kwani kuna mabadiliko makubwa sana kwa manispaa yetu ya kimaendeleo, ambayo hayajawahi tokea na huu ndio utumishi uliotukuka hatuna budi kuwapongeza"amesema Mabushi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura baada ya kupokea vyeti vya pongezi, amesema katika maisha yake hajawahi kupewa pongezi na viongozi wa kiroho,hivyo alichofanyiwa ni muujiza mkubwa katika maisha yake, hivyo ameahidi kufanya mambo makubwa zaidi katika manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na watumishi wenzake.
"Huu ni muujiza mkubwa kwangu,haujawahi kutokea hivyo najikuta naandika historia yangu hii kutokana na ushirikiano wa watumishi wenzangu, nawashukuru sana viongozi wangu wa kiroho,nimekuwa nikipata pongezi kutoka kwa wananchi kwa kupigiwa simu, lakini hiki mlichonifanyia leo nakithamini sana,namrudishia sifa na utukufu mwenyezi Mungu, kwa niaba ya wenzangu tunaahidi kufanya makubwa zaidi na hii ni hatua ya awali tu"amesema Satura.
"Sisi serikali kazi yetu ni kuboresha mazingira na kuona uchumi wa Shinyanga unaongezeka, tuna mpango wa kuufanya mji wa Shinyanga kuwa mkubwa wa kiuchumi, sisi kazi yetu ni kuandaa mazingira shawishi kwa wawekezaji, na tunataka uwe mji wa mfano, heshima ya mtumishi inatoka pale mtumishi anapotoa muda wake, mchango wake katika kumhudumia mwananchi"amesema Satura.
Askofu David Mabushi aliambatana na viongozi wa kanisa hilo akiwemo mwenyekiti wa bodi ya kanisa hilo Lucas Lugwila, Leonard Kajiba, mzee wa kanisa, Sylivester Kahema,Mwinjilist, Emiliana Daniel katibu wa wanawake na Christina Kajala mwenyekiti wa wanawake wa kanisa la IEAGT Shinyanga,ambapo baada ya makabidhiano hayo yalifanyika maombi ya kuombea watumishi wote wa manispaa na Taifa kwa ujumla.
Viongozi wa kanisa la IEAGT Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa manispaa ya Shinyanga
Askofu David Mabushi akikabidhi cheti cha pongezi kwa mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura
Askofu Mabushi akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa manispaa ya Shinyanga
Askofu David Mabushi na watumishi wa manispaa wakiomba baada ya kukabidhiana vyeti vya pongezi
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga akishukuru baada ya kukabidhiwa cheti cha pongezi na Askofu Mabushi
Askofu David Mabushi akimkabidhi afisa utumishi wa manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema cheti cha pongezi kwa ajili ya watumishi wa manispaa
Emiliana Daniel katibu wa wanawake wa IEAGT akiwa na Christina Kajala mwenyekiti wa wanawake IEAGT akisaini kitabu manispaa
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga akimsikiliza askofu Mabushi
Askofu Mabushi akizungumza kabla yakukabidhi cheti cha pongezi
Mzee wa kanisa la IEAGT Leonald Kajiba akipongezana na mkurugenzi.
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa kanisa la IEAGT
Viongozi wa kanisa la IEAGT wakiwa katika maeneo ya ofisi ya Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga
Mzee wa kanisa la IEAGT Leonard Kajiba akiongoza sala fupi ya kuombea ofisi ya Mkurugenzi na watumishi wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464