Kaimu ofisa lishe halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga akieleza kanisani maana ya siku
1000 za mtoto kuanza
kupata lishe bora.
Na Kareny Masasy, Kahama
WAUMINI wa kanisa la kisabato SDA Igomela wilayani Kahama wamepewa somo la lishe katika maandalizi ya ujauzito huaza kabla ya miezi sita na kumtengeneza mtoto aliye bora.
Kaimu ofisa
lishe wa halmashauri ya Msalala wilayani
Kahama Peter Shimba amesema hayo jana kwenye
kongamano la mafundisho ya afya kwa waumini wa kanisa la Kisabato katika kanisa la Igomelo SDA .
Shimba amesema wajawazito
wengi wanapopata ujauzito huanza kusema wanajisikia vibaya hali hiyo inatokana
na mama huyo kukosa maandalizi ya lishe tangu awali kabla ya kubeba ujauzito
huo.
Shimba
amesema baadhi ya mama wengi wanabeba
mimba wanasema ni bahati mbaya dhana
hiyo waondoe wafanye maandalizi ya lishe
kwanza ili kuweza kuwa na mtoto
aliyebora…..
“Kila mzazi
anapenda kuwa na mtoto bora na mtoto bora huanza kutengenezwa kwa kupata lishe bora kabla ya kuzaliwa na
baada ya kuzaliwa ndipo inafikisha siku 1000”amesema Shimba.
Shimba akifafanua
faida za rangi
tano za mboga ya majani na matunda katika mwili ili kuepukana na magonjwa na kuongeza
kinga mwilini.
“Mkoa wa
Shinyanga kwa tafiti zilizotolewa na
Tanzanaia Demographic Health Suvey (TDHS) mwaka 2018 zinaeleza udumavu kwa watoto ni asilimia 32”.
Mzee wa kanisa hilo Bazwanje
Wilbert amesema kanisani hapo huwa wanasomo la afya ambapo leo wamempata ofisa lishe
na kutoa elimu ya lishe wameelewa umuhimi wa afya kwa kipengele cha lishe kwa watoto na wajawazito.
“Ili kuifanya Tanzania kuwa na watoto bora lazima tuwapatie watoto wetu lishe bora na kuhimiza wazazi kunyonyesha muda wa miaka miwili”amesema Wilbert.
Muumini Dinna
Mnyoro ameelewa siku 1000 tangu mama
anapobeba ujauzito na mtaalamu huyo
kufafanua mboga za majani na matunda ni kitu muhimu kwa wazazi nafikiri wamemuelewa vizuri kuwa rangi tano
zote kwenye mboga za majani ni muhimu mwilini.
Waumini wa kanisa la wasabato Igomela SDA wilayani Kahama. mkoani Shinyanga.
Mhudumu wa kanisa la SDA kanisa la Igomelo Yona Machibya akielezea umuhimu wa kongamono kwa kupata elimu za afya mbalimbali.
viongozi wakiwa meza kuu wakijiandaa na kongamano