PROFESA Williamu Mahalu ambaye ni bingwa mbobezi wa upasuaji wa moyo na kifua kutoka Hospitali ya rufaa Bugando.
Na
Kareny Masasy, Bukombe
PROFESA Williamu Mahalu ambaye ni bingwa mbobezi wa upasuaji wa moyo na kifua kutoka Hospitali ya rufaa Bugando amesema wazazi wengi hawatambui matatizo ya moyo kwa watoto wao.
Na kati ya watoto laki moja basi watoto
15 wanakutwa na magonjwa ya moyo hapa nchini.
Profesa Mahalu
amesema hayo jana mbele ya waandishi wa
habari katika hospitali ya binafsi
ya Charles Kulwa Memorial iliyopo Ruzewe wilayani Bukombe mkoani Geita ambapo amekuwa akitoa huduma ya kutibu
Moyo kwa watu wazima na watoto.
Profesa
Mahalu amesema wazazi wengi hawatambui matatizo ya moyo kwa
watoto wao kwani hospitalini hapo amekuwa akiwatibu watu wengi kwa mwezi
wagonjwa wenye matatizo ya moyo
ni 77 hadi 80 kati yao watoto ni asilimia 5.
“Wazazi
wengi hawatambui magonjwa ya moyo kwa watoto wao wengi wanafikiri mtoto
anakikohozi nakumpeleka kwenye vituo vya afya au zahanati hawafikirii kuwapatia
vipimo ili kubaini tatizo mapema”alisema profess Mahalu.
Profesa Mahalu amesema magonjwa ya kuridhi mfano shinikizo la damu mengine yakuyapata kutokana
na desturi ya vyakula vinavyoliwa kwa
kuwekewa mafuta mengi nakufanya
moyo kutanuka na wengine kuzaliwa moyo
na matundu.
“Zamani
walikuwa na imani za kishirikina lakini sio kwamba siku hizi magonjwa mengi
bali yametambuliwa mengi na kufanyiwa
mchakato wa kupata tiba yake”amesema
profesa Mahalu.
Profesa
Mahalu amesema bado watu wanatumia ulaji
wa chumvi usio na utaratibu mzuri nao ni changamoto inayoleta madhara katika
moyo ushauri waepuke ili kuondoa madhara hayo.
‘Wagonjwa
wengi walikuwa wakishindwa kusafiri kwenda Mwanza kupata matibabu ya Moyo lakini hospitali ya Charles Kulwa Memorial imeweza kusogeza huduma hii kwa ukaribu.”amesema profesa Mahalu.
Mkurugenzi
wa hospitali ya Charles Kulwa Memorial dkt Baraka Kulwa
anasema kwa sasa wamekuwa wakitoa huduma za kibingwa kila siku na madaktari wapo zamani ilikuwa
mara moja kwa mwezi.
Kulwa
anasema wagonjwa wamekuwa wakiongezeka kutoka maeneo mbalimbali wenye bima za
afya na wasiokuwa nazo kwani kiwango wanachokitoa ni kama hospitali
ya wilaya na sasa wanataka kupigania ifike kiwango cha mkoa.
Dkt Kulwa
amesema serikali imeweka mazingira
mazuri kwa ushirikiano wa kutoa baadhi ya dawa na vifaa tiba bure kwa lengo la
kutoa huduma ya kliniki kwa baba,mama na mtoto.
Baadhi ya
magonjwa dawa zake tunapewa bure na serikali mojawapo ni kifua kikuu, ukoma ,huduma za
CTC na huduma ya kliniki ya baba na
mtoto (RCH) bure kwani vifaa tiba serikali inatoa ili kuokoa vifo vya mama na
mtoto pia .
Mtaalamu wa masuala ya mionzi (Utralsaound) kutoka hospitali ya Charles Kulwa
Memorial Elmil Mmanyi anawashauri wajawazito mimba inapofikisha
umri wa miezi 20 wapate kuchunguzwa waangaliwe vinasaba vya mtoto kuzuia asipatwe na matatizo ya mdomo sungura,kichwa kikubwa,moyo
na mgongo wazi .
Mmanyi
amesema wapo wajawazito waliofika hapo
na kubainika watoto wao waliopo tumboni wana changamoto lakini ilivyobainika
walianza kupata huduma na tatizo hilo likaondoka.
Mtaalamu wa Mionzi bingwa kutoka hospiatli ya rufaa Bugando Rajabu Kidenda anayetoa huduma kwenye hospitali ya Charles Kulwa Memorial anasema kuwa Utralsound ni mionzi iliyosalama .
Pia kwa siku katika hospitali hiyo huwafanyia
watu 30 hadi 40 wakiwemo wajawazito na
wiki moja hutoa elimu mara mbili juu mionzi hiyo.
Eneo la Hospitali ya Charles Kulwa Memorial
eneo la chumba cha upasuaji katika hospitali ya Charles Kulwa Memorial
Mtaalamu wa meno katika hospitali ya Charles Kulwa akiwa kazini
Mtaalamu wa maabara Yusuph Hashimu akiwa kazini katika hospitali ya Charles Kulwa Memorial
Profesa Williamu Mahalu ambaye ni bingwa wa magonywa ya moyo na kifua kitoka hospitali ya rufaa ya Bugando ambaye amekuja kutoa huduma za kibingwa katika hospitali ya Charles Kulwa Memorial
Mkurugenzi wa hospitali ya Charles Kulwa Memorial dkt Baraka Kulwa akiwa kwenye chumba tayari kutoa huduma.
Mtaalamu wa mionzi (ultrasound) kutoka hospitali ya rufaa ya Bugando Rajabu Kidenda akiwa katika hospitali ya Charles Kulwa Memoriali akitoa huduma. Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464