Mkurugenzi wa shule KOM -Class Jackton Koyi akizungumza kwenye mahafari ya pili ya shule ya msingi KOM
Suzy Luhende,Shinyanga blog
Wanafunzi wa shule binafsi ya msingi inayomilikiwa na kampuni ya Kom-Class Ltd, ambayo ipo eneo la Butengwa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga,wamefanya mahari ya pili ya kuhitimu darasa la saba ikiwa ni pamoja na kuagwa kwa wanafunzi wa darasa la awali kuingia darasa la kwanza.
Mahafari hiyo imefanyika leo Octoba14,2022 shuleni hapo,ambapo wamehitimu wanafunzi 36 na watoto wa awali kuagwa ili kuendelea na darasa la kwanza.
Katika mahafali hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Eng. Peter Kuguru ambaye ni mjumbe wa bodi ya shule ya KOM sekondari, amewataka wazazi wandelee na juhudi za kuwasomesha watoto wao ili waweze kutimiza ndoto zao.
"Nawapongeza sana wazazi, kwa kuwaleta mahali hapa watoto wenu nimesikia na kuwaona watoto wa shule ya awali wakisoma risala kwa kingereza hiyo, inaonyesha wanafunzi wetu wanaandaliwa vizuri, naomba wazazi wote walete watoto hapa kwenye elimu bora, inaonyesha walimu wanafundisha vizuri na kwa umakini,"amesema Kuguru.
"Kweli nimejionea mwenyewe kila mtoto anajieleza kwa ujasiri, na wanalelewa kulingana na dini zao,walimu wanaonekana ni wabunifu sana na ukiwaangalia vitu wanavyovifanya hapa si vya kukariri ni vya kuelewa kabisa,"ameongeza Kuguru.
Amesema amesikia kwenye risala kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya wazazi kutolipa kwa wakati ada, hali ambayo inawafanya watoto wasifike kwa wakati shuleni, hivyo amewaomba wazazi walipe kwa wakati kama wanakwama ada wazungumze na wahusika wa shule ili watoto wasipitwe na vipindi.
"Wazazi nawaomba muache kuwachelewesha watoto majumbani wakati wa likizo kama umekwama ada njoo zungumza na menejmenti mtoto aendelee na vipindi vya masomo,tunafanya dhambi kubwa sana kwa watoto wetu kuwachelewesha kuwaleta shuleni jitahidini ndugu zangu wazazi, mkakati wa shule mtoto mtoto afaulu vizuri"amesema.
Akisoma risala ya shule hiyo mwalimu mkuu Derick Okech amesema Changamoto nyingine ni tozo nyingi za serikali, kupanda kwa bei ya chakula, kupanda kwa bei ya mafuta ya kwenye magari awali walikuwa wakitumia sh 4 milioni kwa mwezi mzima, lakini kwa sasa wanatumia Sh 10 milioni pia mzazi kutotoa taarifa ya kuumwa kwa mtoto.
Shule ya Awali na Msingi KOM ilianzishwa Januari, mwaka 2016 ikiwa na jumla ya wanafunzi 48, walimu 5 na wafanyakazi wasio walimu 4, hivyo ina mafanikio mazuri kitaaluma na malezi vimewezesha shule hiyo kukua kwa kasi ambapo hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 507, walimu 25 na wafanyakazi wasio walimu 19.
Wakati wanafunzi wa madarasa ya chini kuanzia darasa la awali hadi la nne wakisoma kwa kutwa, wanafunzi wa darasa la tano hadi la saba huishi bweni kwa lengo la kuwapa wanafunzi na walimu muda wa kutosha wa mazoezi na masomo ya ziada.
Okech ametaja Dira kuu ya shule hiyo ni kuweka mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia ili kuwezesha wanafunzi kufikia ndoto na malengo yao kielimu na kimaisha.
“Msingi wetu mkuu ni kuwajengea wanafunzi wetu uwezo kamili kielimu, kuwapa maarifa na ujuzi utakaowawezesha kumudu ushindani katika soko la ajira ndani na nje ya nchi, na lengo letu siyo tu ufaulu katika majaribio na mitihani, bali pia ni kuwafanya wahitimu wetu kupata ujuzi na maarifa ya kumudu maisha yao sasa na baadaye, wakitumia nyenzo na fursa zinazopatikana katika mazingira yao,”
Okech amesema ili kufikia malengo hayo, moja ya msingi mkuu ni kuwaandaa na kuwajengea wanafunzi wote uwezo wa kujiamini, kujiheshimu wao binafsi na kuwaheshimu wengine na hatimaye kujenga jamii na Taifa la watu wenye weledi na maadili mema.
“Tunataka vijana wetu wanaohitimu hapa, siyo tu wanakuwa raia wema, bali pia wenye mchango chanya katika jamii na Taifa kwa ujumla,” amesema Okech
Katika kufanikisha malengo hayo, Mwalimu Mkuu huyo amesema walimu wa shule hiyo hutumia mbinu za kisasa za ufundishaji shirikishi ndani na nje ya darasa unaotoa fursa kwa wanafunzi kujieleza, kutoa maoni yao na kufanya kwa vitendo yote wanayofundishwa nia ikiwa ni kuwajengea uelewa zaidi.
"Shule yetu imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika nyanja zifuatazo kitaaluma, kwani shule inatumia mbinu za kisasa na shirikishi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji, na hapa kwetu watoto wanashirikishwa ipasavyo katika hatua zote za kujifunza ndani na nje ya darasa; tunafundisha kwa nadharia na kwa vitendo. Mbinu hii huwawezesha wanafunzi siyo tu kuelewa, bali pia kupata ujuzi na maarifa zaidi. Hii ni miongoni mwa siri ya mafanikio yetu” amesema Mwalimu huyo.
Amesema licha ya kuwapa wanafunzi wake ufaulu mzuri wa daraja “A” na “B” katika matokeo ya mitihani ya kitaifa ya darasa la nne na la saba kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2021, mbinu hiyo pia inawapa matumaini ya kufanya vema zaidi katika matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka huu.
"Katika matokeo ya kitaifa ya darasa la saba mwaka 2021, shule yetu ilishika nafasi ya tatu kiwilaya, kimkoa tulikuwa wa 19 huku kitaifa tulishika nafasi ya 324, mikakati yetu ni kushika nafasi ya kwanza kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa hadi Taifa,” anasema Mwalimu Okech.
“Licha ya mbinu ya ufundishaji, mafanikio ya shule yetu pia inachangiwa na uwepo wa Miundombinu rafiki ya kufundishia na kujifunzia ikiwemo vyumba vya madarasa, ofisi na nyumba za walimu, jengo la utawala, bwalo la chakula na mabweni,” anasema Okechi
Shule ya Kom pia ina maktaba iliyosheheni vitabu vya ziada na kiada, ukumbi wa mikutano na shughuli za kijamii bila kusahau chumba cha elimu ya kompyuta, pia kuna vyumba vinne vya madarasa ya awali, vyumba 15 kwa madarasa ya msingi (darasa la kwanza hadi la saba) na mabweni manne kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la tano hadi la saba waishio bwenini.
Huduma ya nishati ya umeme ni jambo muhimu kwa ajili ya shughuli za kimasomo, ulinzi na usalama kwa jamii ya shule ndio maana uongozi umehakikisha kuwa, licha ya kuunganishwa kwenye gridi ya Taifa ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco), pia kuna jenereta kwa ajili ya dharura yoyote.
"Eneo lote la shule hii limezungushiwa uzio wa ukuta ili kuongeza usalama wa mali, wanafunzi na jumuiya nzima ya shule ina huduma ya uhakika wa maji, ni eneo lingine muhimu ndio maana licha ya kuunganishwa kwenye mtandao wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria, pia tunacho kisima kirefu chenye uwezo wa kutuzalishia maji zaidi ya lita za ujazo 5, 800 kwa saa; hii imetufanya tusiwe na changamoto ya maji,” amesema.
Okech amesema katika suala la usafiri ni eneo lingine la kipaumbele, ndio maana uongozi wa shule ya awali na msingi KOM umenunua mabasi matano kwa ajili ya kusafirisha watoto wa kutwa watokao na kurudi nyumbani.
"Tuna viwanja vya michezo mbalimbali kuanzia soka, mpira wa wavu, pete kutokana na kutambua umuhimu wa michezo shuleni. Tunayo pia eneo la michezo yote muhimu kwa watoto ikiwemo bembea za aina tofauti tofauti," ameleza Okech.
"Kwa keeli mazingira yetu ni mazuri na mandhari ya kuvutia ya shule yetu ni miongoni mwa mambo ya kujivunia kwa sababu siyo tu yanawavutia watoto, bali pia huwafanya waishi kwa furaha. Pia tumepanda aina mbalimbali za miti ya matunda, maua na kivuli,”amesema Okech.
Kwa pande wake mkurugenzi wa shule hiyo Jackton Koyi amemshukuru Rais wa jamhuri ya muungano Samia Suluhu kwa kutoa fadhili kwa wanafunzi 600 ambao kati ya hao wapo wanafunzi watatu waliohitimu kutoka shule ya KOM Shinyanga,hivyo amewaomba wazazi waendelee kiamini ili iendee kutimiza maono makubwa zaidi.
Akisoma risala ya darasa la saba Anneth Mkina amesema wanawashukuru walimu wa shule hiyo kwa kuwafundisha vizuri na kuwafanya kuwa na ujasiri, pia wanawashukuru wazazi kwa kuwasomesha, hivyo wamewaomba tena ijapokuwa hali ni ngumu wasiche kuwaendeleza ili waweze kutimiza ndoto zao.
Mkurugenzi wa zhule ya KOM akivalishwa uwa kabla ya kuingia ukumbini
Wanafunzi wa darasa la awali wakicheza
Mkurugenzi wa Shule ya KOM Jackton Koyi akizungumza kwenye mahafali ya pili ya darasa la saba
Wahitimu wa darasa la saba shule ya msingi KOM wakijiandaa kuingia ukumbini
Wahitimu wa darasa la saba shule ya msingi KOM wakiingia ukumbini
Wahitimu wa darasa la saba shule ya msingi KOM wakicheza
Mkurugenzi akiwa na waalimu wakuu wa shule ya KOM
Wanafunzi wa shule ya KOM wakicheza ngoma ya kisukuma
Wanafunzi wa shule ya KOM wakicheza ngoma ya kisukuma
Wanafunzi wa shule ya Msingi KOM wakicheza ngoma ya Kijaruo
Mkurugenzi wa KOM akizungumza kwenye mahafari ya pili ya darasa la saba
Wahitimu darasa la awali wakiwa kwenye picha ya pamoja
Meneja wa shule hiyo Magreth Koyi akimpongeza mwanafunzi kwa kuhitimu darasa la saba
Mmoja wa wahitimu akipongezwa kwa kuhitumu darasa la saba
Mmoja wa wahitimu darasa la saba akichukua cheti
Mkurugenzi wa shule ya M
msingi KOM Jackton Koyi kulia ni meneja wa Shule hiyo Magreth Koyi
Mgeni rasm akiwa pamoja na mkrugenzi, meneja wa Shule hiyoagreth Koyi na wageni waalikwa katika mahafari hiyo
Mgeni rasmi wa mahafari ya pili ya shule ya msingi na awali Eng Piter Kuguru akizungumza
Mgeni rasmi wa mahafari ya pili ya shule ya msingi na awali Eng Piter Kuguru akizungumza
Wahitimu wa darasa la saba shule ya msingi KOM wakijiandaa kuingia ukumboni