Mshindi wa kiti cha uenyekiti wilaya ya Kahama kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Thomas Muyonga akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua kwa kura nyingi.
Na Kareny Masasy, Kahama
THOMAS Muyonga ameshinda nafasi ya mwenyekiti wilaya ya Kahama kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 1,722 dhidi ya wapinzani wake Costantine Makoye aliyepata kura 179 na Michael Kulwa aliyepata kura 127.
Uchaguzi huo
ulianza jana tarehe 1 mwezi October na
kukamilika leo tarehe 2 mwezi October
mwaka 2022 kwa kuendelea kuchagua kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya wilaya huku wajumbe takribani 2028 walijitokeza kupiga kura kwa nafasi ya
mwenyekiti wilaya.
Msimamizi wa
uchaguzi huo James Kusekwa ametangaza matokea na majina ya waliojitokeza kugombea
nafasi mbalimbali ambapo alimtangaza
mwenyekiti Thomas Muyonga kuwa mwenyekiti wa CCM wilaya baada ya kutetea kiti hicho kwa awamu ya pili sasa.
Kusekwa amemtangaza
katibu wa siasa itikadi na uenezi Joackim
Simbila aliyetetea kiti hicho kwa kupata kura 151 dhidi ya wapinzani wake Mola Zabron aliyepata
kura 72 na Ambrose Nkwabi aliyepata kura 44 huku wajumbe waliopiga kura kwenye nafasi hiyo wakiwa 267.
Aidha Kusekwa
aliendelea kutangaza makundi ya uwakilishi ambapo kundi la vijana mshindi
alikuwa Godfrida Simba aliyepata kura 261
kati ya kura 263, kundi la wazazi Julias
Lugobi aliyepata kura 203 huku kundi la uwakilishi
umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi
(UWT)
alichaguliwa Juliana Kajala.
Baada ya
kutangwa kwa matokeo hayo mshindi Thomas Muyonga alipata nafasi ya kuwasalimia wajumbe nakueleza kuwa
uchaguzi umekwisha wanatakiwa wasonge mbele kazi iendelee na kuvunja makundi
yaliyokuwepo.
Muyonga amewashukuru wajumbe kwa kuwa wavumilivu kwa zoezi la uchaguzi lililoanza jana na kumchagua kuendelea kuongoza kiti hicho kwa kipindi cha miaka mitano tena.
Wajumbe wakiwa ukumbini wakisubiri maelekezo.Uchaguzi wilayani Kahama.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya walipokuwa kwenye uchaguzi.
Mwenyekiti wa Thomas Muyonga akiwa meza kuu na msimamizi wa uchaguzi James Kusekwa.
Mwenyekiti Thomasi Muyonga baada ya kuchaguliwa na kushinda akisumbiri matokeo ya kamati ya utekelezaji
Wajumbe wakimbeba katibu wa siasa itikadi na uenezi Joackim Simbila baada ya kutangazwa mshindi.
Wajumbe wakimbeba katibu wa siasa itikadi na uenezi wilayani Kahama Joackimu Simbila
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama baada ya ushindi akiongea kwa kuwashukuru wajumbe kumchagua tena kwa awamu ya pili.