TRA -MKOA WA KIKODI KAHAMA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUTUNZA KUMBUKUMBU ZAO.


Baadhi ya wafanyabiashara  halmahsuari ya Ushetu wakimsikiliza afisa msimamizi wa kodi kanda ya ziwa  kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Morgan Isdory.

Na  Neema Sawaka, Kahama

MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA)  mkoa wa kodi Kahama Imewataka wafanyabiashara  kutunza kumbukumbu zao  za biashara    kwa mujibu wa sheria ya fedha ya  mwaka 2022 .

 Afisa msimamizi  wa kodi kutoka  kanda ya ziwa Morgan Isdory  amesema hayo   jana wakati akitoa elimu ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara wa halmashauri ya Ushetu.

Isidory  amesema  wapo pia wafanyabiashara ambao wamekuwa  na mashine za EFD na kutotoa risiti kabisa kwa mteja  na wengine kutoa bei pungufu kwenye bidhaa tofauti na uhalisia hilo ni kosa na faini yake ni kifungo cha miaka mitatu au kulipa sh Millioni tatu.

Isdory amesema nchi zilizoendelea ukwepaji wa kodi ni kosa la jinai  ndiyo maana hapa Tanzania mara kwa mara kumekuwepo maboresho ya kanuni na sheria.

Isdory amesema  kwa mujibu wa sheria ya fedha ya  mwaka 2022  inaeleza kodi itatozwa  kwenye faida  kwa mfanyabiashara  awe na uwezo  wa kutunza kumbukumbu.

“Uzingatiaji  wa  kifungu  cha 35 cha sheria ya  usimamizi wa kodi na utunzaji wa kumbukumbu ni muhimu kwa kumfanyabiashara”amesema Isdory.

Isdory amesema  mfanyabiashara asiye na kumbukumbu makadirio yanaweza  kuwa sahihi au  yasiwe sahihi kwake.

Isdory amesema  kanuni za kodi zinaeleza gharama ya usafirishaji  haitakiwi kuzidi   kodi anayotakiwa kulipa mfanyabiashara.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhulia kupata elimu hiyo  Msabaha Issa na  Ramadhani Ngau wamesema kodi zimekuwa nyingi  kwa mfanyabiashara zingine zipunguzwe ili wapate faida.

 

Wafanyabiahsra halmahsuari ya Ushetu wakimsikiliza afisa msimamzi wa kodi kanda ya ziwa  kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Morgan Isdory.

Wafanyabiahsra halmahsuari ya Ushetu wakimsikiliza afisa msimamzi wa kodi kanda ya ziwa  kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Morgan Isdory.

Mfanyabiashara  Msabaha Issa akiongea kwenye semina 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464