Wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Nyandekwa manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Na mwandishi wetu
Wazazi kata ya Nyandekwa manispaa ya Kahama wametakiwa kushirikiana na serikali ili kuondoa changmoto zinazowakabili wanafunzi na walimu shuleni ikiwemo ujenzi wa matundu ya vyoo na nyumba za walimu.
Mgeni
rasmi Emanuel Ntonge ambaye ni mstaafu wa chuo cha uhasibu Tabora ameyasema hayo jana kwenye mahafali ya 13 ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Nyandekwa.
Ntonge amewataka wahitimu wanapo kuwa nyumbani wawe na maadili mema na kutojiingiza kwenye makundi maovu.
Ntonge
amewataka wanafunzi wanaobaki kuachana na tabia za utoro nakuwasihi
wasome kwa bidii ili kuweza
kufikia malengo yao kwani ada na
michango mingine imeondolewa na serikali.
Mkuu wa
shule hiyo Kiseka kallam amesema kuna wahitimu 90 kwa mwaka huu na wamejipanga vyema kufanya mtihani mwezi ujao.
Aidha risala ya wanafunzi iliyosomwa na Magreth Elias wameomba serikali masomo yafundishwe kwa lugha ya Kiswahili ili waweze kuelewa.
Mgeni rasmi akiingia nakuwasalimia waalikwa
Wahitimu wakisikiliza wosia kutoka kwa mgeni rasmi
Mhitimu akisoma risala
Mgeni rasmi Emanuel Ntonge akipokea risala kutoka kwa wahitimu
Wahitimu wa kidato cha nne wakiingia ukumbuni
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464