WATENDAJI WA KATA HALMASHAURI YA MSALALA WASAINI MKATABA WA LISHE




Watendaji wa kata  wakiwa kwenye zoezi la kusaini mikataba ya lishe katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

 Na Kareny  Masasy,Msalala

WATENDAJI wa kata 18 za halmashauri ya Msalala  wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamesaini mikataba ya utekelezaji  shughuli za lishe ili kuwakomboa wajawazito na watoto.

Mikataba hiyo wamesainishwa leo tarehe 19/10/2022 na mkurugenzi wa halmashauri  hiyo Charles Fussi  mbele ya ofisa mratibu wa shughuli za lishe mkoa Denis Madeleka.

Fussi amesema kuwa mkataba huo unajieleza watendaji wakafanye kazi  na kusimamia kuanzia ngazi ya  kata,vijiji na vitongozi kuhakikisha walengwa wanapata huduma  na ushauri.

Mratibu wa Lishe  Denis Madeleka  amesema kuwa mkataba huo unaviashiria  nane,kiashiria cha kwanza ni kwenda  kwa walezi wenye watoto waliochini ya umri wa miaka mitano  na wajawazito kutoa elimu ya lishe na kuandaa ripoti .

‘Hapa msalala kuna vituo vya kutolea huduma takribani 30 pia kuna fomu ambazo watakuwa wakizijaza  kupitia vituo hivyo kwa kushirikiana na wasimamizi wa lishe kwenye vituo na watoa huduma ngazi za jamii ambao walikwisha patiwa mafunzo”amesema Madeleka.

Madeleka amesema matone ya vitamin A ,utolewaji wa dawa za minyoo ,na utolewaji wa dawa za Follic Acid kwa wajawazito wakasimamie na wajue  bajeti yake ni sh ngapi  na taarifa hizi zianze kutolewa kwenye vikao vya maendeleo ya kata (WODC).

Mdeleka amesema watoto wenye utapiamlo  wa kadiri na mkali  waibuliwe  na kutolewa taarifa zao na kupelekwa kwenye vituo wakapatiwe matibabu  pia kuna muongozo umeandaliwa wa wanafunzi kuanza kupata chakula cha mchana  shuleni kupitia  kamati zitakazo kuwa zinasimamia.

Kaimu  afisa lishe halmashauri ya Msalala Peter Shimba amesema wameonekana kufanya vibaya suala la lishe kwenye eneo la shule kwaajili ya kutopata watoto chakula mashuleni hilo nalo lisisitizwe kwa wazazi ili wasiwe na alama mbaya.

Elimu muende mkaitoe kwa kuainisha makundi  matano ya vyakula   na umuhimu wake mwilini  kwani watoto wakipata afya njema hata uelewa unakuwa mzuri darasani na kuwepo na taifa imara.

Mtendaji wa kata ya  Bugarama Prisca Pius amesema mkataba huo wameupokea na wataufanyia kazi kama ilivyoelekezwa kwa kushirikiana na wahudumu ngazi ya jamii pamoja na wahudumu wa lishe kwenye vituo afya.


Mratibu wa lishe mkoa wa Shinyanga  Denis Madeleka  akiongea  juu ya mikataba hiyo kwa watendaji wa kata.

Mtendaji wa kata akisaidni mkataba.  

Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala  Charles Fussi akiangalia mkataba.



Mtendaji wa kata akipokea mkataba

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464