WENYE UALBINO WAPEWA MRADI NA KUTOA BIMA ZA AFYA YA CHF

   WENYE UALBINO WAPEWA MRADI NA KUTOA BIMA ZA AFYA YA CHF

 
Picha ya watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija -Shinyanga.


 

 Na Shaban Njia, KAHAMA.

 

CHAMA cha Watu wenye Ualbino (TAS) Wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kimepewa mradi jumuishi kwa watu wenye ualbino wenye thamani ya Sh. milioni 90 na Shirika lisilo la kiserikali la Karagwe Community Based Rihabiltation Programe (KCBRP) na kutoa elimu kwenye jamii.

 

Mradi huo ulitekelezwa katika Halmashauri ya Msalala kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 hadi mwaka 2020/2021 na kila mwaka walikuwa wakipewa kiasi cha Sh.milioni 30 na walikuwa wakitekeleza katika Halmashauri ya Msalala pekee.

 

Kadhalika, mradi huo uliwawezesha wenye ualbino kupata elimu ya ujasiriamali, elimu kwenye jamii kuhusu ualbino pamoja kutoka Bima za afya ya CHF iliyoboreshwa kwenye kaya 30 zenye ualbino wasiojiweza kwa muda wa mwaka mmoja hali iliyofanya kupata matibabu bure katika vituo vya afya.

 

Mwenyekiti wa Chama hicho Nisha Phabian aliyabainisha hayo wakati akizungunza na vyombo vya habari alisema hata wao wanaweza kupata miradi mikubwa kuitekeleza na kutoa elimu kwenye jamii juu ya kutokomeza vitendo vya mauaji kwa watu wenye ualbino.

 

Alisema, kila mwaka wakati wa utekelezaji wa mradi huo walikuwa wakipewa Sh. milioni 30 na shirika hilo na waliutekeleza vema na jamii ilipata elimu sahihi namna ya kushirikiana na watu wenye ualbino katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na wamenufaika wote kupitia mradi huo.

 

Pia alisema, katika utekelezaji wa mradi huo walishirikisha jamii ya halmashauri nzima ya Msalala hususani wale wanaoishi pembezoni na kuendekeza mila potofu juu yao, kwamba wanaposhikana mikono au kusalimia na mtu mwenye ualbino ni mkosi na huwezi kupata mali jambo ambalo sio kweli.

 

Nae Omary Abdarahamani mkazi wa Mwanase alisema, awali kabla ya kupata elimu ya namna ya kushirikiana na watu wenye ualbino kwenye shughuli za kiuchumi walikuwa wakiwatenga wakiani wakiwa nao watashindwa kutimiza ndoto zao jambo ambalo sio kweli baada ya kupewa elimu.

 

Alisema, kutokana na kupewa mifano mbalimbali ya watu wenye ualbino waliofanikiwa kimaisha hususani vipongozi wa serikali iliwafanya kuona nao wanahaki ya kuwa nao na kuhakikisha wanakuwa pamoja katika kufanya ujasirimali na sasa vitendo vya mauaji juu yao vimeondoka kabisa.

 

Kwa upande wake, Beatrice Mabula alisema,mila potofuli ndio ilikuwa inawafanya kushinwa kushirikana na wenye ualbino kwani kipindi cha ukuaji wake aliaminishwa akiwa karibu nao na yeye anaweza kuzaa mtoto wenye ualbino lakini elimu hiyo ilifumbua kifikra na kuona ni uongo ulikuwa umejengeka kwa wazee wao.

 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464