WFT-T,C4C,SERIKALI,JAMII & WADAU
SHINYANGA,WAJADILI UTAFITI WA KUTUMIA MBINU ZA ASILI KATIKA KUTOKOMEZA UKATILI.
Na mwadishi wetu.
Wadau, serikali na jamii mkoa wa Shinyanga wamekutana katika kufanya majadiliano ya kutambua mbinu sahihi za kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa mkoa wa Shinyanga.Mjadala huo ulijadili juu ya mbinu za asili katika mila na desturi za wakazi wa mkoa wa Shinyanga zinazoweza kusaidia kutokomeza ukatili kupitia utafiti wa hatua ya tatu ulioasilishwa na shirika la Citizen for Change (C4C)
Kikao kazi cha majadiliano( Prototype event session) kimefanyika kwa siku tatu kati ya tarehe 10-hadi 12 oktoba,2022 katika hoteli ya karena iliyopo manispaa ya Shinyanga kwa kuratibiwa na Taasisi ya Mfuko wa Wanawake Tanzania(WFT-T) kwa ufadhili wa shirika la Citizen for Change(C4C). Kikao hicho kilishirikisha wadau kutoka sekta binafsi ambapo ni Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Rafiki Sdo,Redio Faraja,Yawe,Weado,Thubutu,Ywl,Gci,Agape na kwa upande wa Serikali ni, Jeshi la polisi Shinyanga, ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Pia, mjadala huo ulikuwa na ushiriki wa makundi mbalimbali ndani ya jamii ambao ni pamoja na waalimu,viongozi wa jeshi la jadi sungusungu,wazee wa mila,wenyeviti wa vijiji,Viongozi wa dini na wawakilishi kutoka baraza la watoto.
Mratibu na wa Mfuko wa Wanawake Tanzania kwa mkoa wa Shinyanga ,Groly Mbia alisema wamewaita wadau hao ili kuweza Kujadili hatua ya tatu ya utafiti unaofanywa na shirika la Citizen for Change katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kuweza kupata mikakati ya itakayosaidia kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Tumewaita hapa kwa
lengo la kuendelea kujadili hatua ya utafiti unaofanywa na wenzetu ili kuweza
kutambua mbinu za kiasili zilitozo tajwa na wanajamii zinazoweza kusaidia
kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto,Tuko hapa kwa ajili ya kuboresha
na kujadili kwa upanda ni mikakati gani inayoweza kuwa rahisi kutokomeza
ukatili katika mkoa wa Shinyanga"Alisema Groly Mbia
Naye Mtafiti na Mkurugenzi wa shirika la Citizen for Change, Dkt. Kate McAlphine alisema kuwa ni wajibu kuchukua maoni na busara za wadau wanaopambana na ukatili kwa mkoa wa Shinyanga katika hatua hiyo ya tatu ya utafiti ili kuweza kujaribu njia zilizosemwa na wanajamii wenyewe ambazo zitasaidia kutokomeza ukatili
“Utafiti huu umeshiriksha jamii husika na wametoa mapendekezo yao na tumeleta kwenu kama wadau muhimu ili kuweza kuboresha na kupata mbinu zitahiki zinazoweza kupambana na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia maoni na busara kutoka kwenu ”Alisema Dkt.Kate.
Kwa upande wake, Afisa maendeleo mkoa wa Shinyanga, Rehema Edson akiwakilisha serikali alisema, Lengo letu ni tuweze kujadili njia zao za asili ambazo zitasaidia katika kutokomeza vitendo vya ukatili kwa kuweza kuboresha hizo mila na desturi zao bila kuwaleta vitu vipya ambavyo ni ngumu katika mapambano haya.
“Bado mila na desturi ni changamoto ya kuchochea vitendo vya ukatili katika mkoa wa Shinyanga na tunapaswa kutumia hizo njia zao za asili ili kuweza kuwa na kazi rahisi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Ipo nuru inaonekana kwa sasa, tofauti na miaka 10 ya huko nyuma ambapo mabadiliko yanaonekana kwa wanawake na watoto kwa kupata thamani katika elimu na afya”
Pia, Afisa mradi kutoka shirika la YAWE,Bwana Deus Lyakisi, alisema anayo furaha yake kuona dunia yenye salama na amani kwa wanawake na watoto kwa kushirikiana na wadau wengine katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha, Aisha Omary, Afisa maendeleo wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga alisema anayofuraha katika mabadiliko katika jamii kwa sasa kutokana na nguvu ya wadau katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi na mtafiti kutoka shirika la Citizen for Change(C4C),Dkt Kate McAlphine akizugumzia utafiti wa uliotoka katika jamii kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Neema Msangi kutoka WFT-T akizugumzia muhimu na thamani ya uwekezaji juu ya watoto.
Mratibu wa MTAKUWWA wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Aisha Omary akizungumzia umuhimu wa mjadala.
Raphaeli Deris mwezeshaji kutoka C4C akito maelekezo ya ufafauzi juu ya majadiliano.
Timu ya Citizen for Change ikipeana maekelezo katika kikao.
Mabalozi wa kupambaa na ukatili kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyaga wakijadili mbinu za kutomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Amina Hamis ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la watoto katika shule ya msingi Puni akiwasilisha hoja kwa niaba ya kundi lake
Wawakilishi kutoka baraza la watoto wakiwasilisha hoja zao juu ya mbinu za kutokomeza ukatili.
Mwl.Jovinus Joseph kutoka shule ya msingi Tinde (B) akiwasilisha hoja kwa niaba ya kundi lake
Majadiliao yakiendelea katika vikundi.
Picha zote kwa hisani ya shirika la Citizen for Change