ASASI ZA KIRAIA ZIFANYE UTAFITI KATIKA MILA & DESTURI KUFANIKISHA HARAKATI ZA UFEMINISTI.
Rebecca Mjema Kisenha Mwezeshaji wa wa masuala ya ufeministi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464
Na Mwandishi wetu.
Asasi za kiraia zinazopamba na kutomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga zimeshauriwa kufanya utafiti zaidi katika kuweza kuboresha mikakati na mipango ya ufeministi ili kuwakomboa wanawake wa pembezoni.
Hayo yameelezwa leo jumatano 16,Novemba,2022 na Rebecca Mjema ambaye ni mwezeshaji wa mafunzo y ya ufeministi yaliyofanyika katika hoteli ya Karena Manispaa ya Shinyanga,ambapo asasi za kirai zipatazo 28 za mkoa wa Shinyanga zimeshiriki mafunzo hayo.
Rebeca Alisema,Ni wakati wa wadau kuvaa uhalisia wa maisha halisi ya wanawake na watoto wa pembezoni kwa kufanya utafiti wa mila na desturi za walengwa.
" Mila na desturi ni zimebeba dhamana kubwa ya walengwa na ndani ya jamii zipo mila na desturi ambazo ni mbaya na nzuri,Hivyo wajibu wetu kuzifanyia kazi zile ambazo ni mbaya zinazo wakandamiza wanawake na watoto.Alisema Rebecaa.
" TAPO lenu la SHY-EVAWC kila moja ana rasilimali kwa shirika lake katika kuweka umoja wenye nguvu wa kuweza kuwa na mbinu na mipango bora na imara kwa kuweza kuwakomboa wanawake na watoto dhidi ya ukatili"
Naye,Charles Deogratius wa shirika la WAYDS alisema ni mila na desturi zimekuwa zinabadilika ni wakati wa kuzitambua ili kuweza kuwa na utekelezaji rahisi wa shughuli zetu.