RUWASA SHINYANGA WATENGA BAJETI BILIONI 9.8 KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI KWA WANANCHI


Meneja wa RUWASA mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela akizungumza na wanadishi wa habari hawapo pichani baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa nusu mwaka wa jumuiya za watumia maji Kahama.

Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa nusu mwaka wa jumuiya za watumiaji maji wilaya ya Kahama

Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa nusu mwaka wa jumuiya za watumiaji maji wilaya ya Kahama.

Mkuu wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga akimkabidhi Kompyuta Rehema Juma kiongozi wa jumuiya za watumia maji kutoka kata ya Nyakende kompyuta

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akiendelea kutoa Kompyuta kwa viongozi wa vyombo vya watumiaji maji ngazi za jamii.

Na Salvatory Ntandu

KAHAMA

Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) mkoa wa Shinyanga umetenga bajeti ya shilingi bilioni 9.8 katika mwaka wa fedha 2022/23 kwaajili ya kutejenga miradi mbalimbali ya maji ambayo inatarajiwa kuwanufaisha wakazi zaidi ya laki 2 wanaoishi katika maeneo ya vijijini.
 
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa RUWASA mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela kwenye mkutano mkuu wa nusu mwaka wa jumuiya za watumia maji uliofanyika katika wilaya ya Kahama na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo,madiwani na viongozi wa serikali na chama.

Amesema kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji ikiwa ni pamoja na kuchimba visima virefu,kusambaza huduma ya maji katika vijiji ili kuhakikisha wananchi wanaoishi katika maeneo ya vijijini wananufaika na huduma ya maji safi na salama.

“Mpaka sasa tuna miradi 19 inayoendelea kutekelezwa katika maeneo ya vijijini yenye thamani ya shilingi bilioni 35 fedha ambazo zimetolewa na Rais Samia kwaajili ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani hivyo sisi kama RUWASA tutahakikisha tunawasimamia wakandarasi ili watekeleze miradi hiyo kwa kiwango kinachotakiwa,”amesema Payovela.

Sambamba na hilo Mhandisi Kayovela alisema serikali inatarajia kuanza usanifu wa ujenzi wa mradi wa maji kutoka Kahama kwenda katika halmashauri ya Ushetu ili kuhakikisha wakazi wa maeneo hayo wanaodokana na tatizo la kutumia maji yasiyosafi na salama.

“Halmashauri ya Ushetu inachangamoto katika utafutaji wa vyanzo vya maji maeneo mengi ukichimba visima maji hayapatikani ndio maana serikali imekubali ombi la kupeleka maji ya ziwa viktoria ili waondokana na tatitozo la ukosefu wa huduma hiyo hususani nyakati za kiangazi,”alisema Kayovela.

Kwa upande wake mgeni Rasmi katika mkutano huo mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga aliiagaiza RUWASA kuhakikisha inawasimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji ili ikamilike kwa wakati ili kuwaondolea adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.

“Serikali haitamvumilia mkandarasi wa maji ambaye atabainika kuchelewesha mradi bila sababu yeyote ya msingi, Rais Samia analeta fedha nyingi ili kumtua mama ndoo ya maji lakini wapo baadhi ya wakandarasi wanachelewesha miradi kwa makusudi tukimbaini tutachukua hatua kali za kisheria dhidi yake,”amesema Kiswaga

Naye Selina Maziku mwenyeki wa jumuiya za watumia maji ya Nyankende aliiomba RUWASA kuongeza usambazaji wa maji katika miradi wanayoitekeleza ili kutoa fursa kwa wananchi wa vijiji husika kunufaika na mradi hiyo.

Katika mkutano jumuia za watumia maji walipatiwa thamani za ofisi zikwemo kompyuta ili kuwarahisishia kazi zao ambazo zinathamani ya zaidi ya shiligi milioni 5.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464