Hatari mikopo ‘kausha damu’
Dar es Salaam. Ongezeko la taasisi zinazotoa mikopo ‘chap chap’ yenye riba kubwa na kugeuka machungu kwa wakopaji, imeelezwa kuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwa mdaiwa, kufariki kwa shinikizo la damu au kukimbia kusikojulikana.
Mikopo hiyo iliyopachikwa jina la ‘kausha damu’ kutokana na maumivu wanayopata wakopaji wakati wa kurejesha fedha, baadhi ya taasisi zimekuwa zikitoa masharti magumu, ikiwamo kutaifisha mali zikiwemo nyumba, magari na samani za ndani endapo mhusika atashindwa kulipa kwa wakati.
Uchunguzi uliofanywa na Mwanachi umebaini kuwa wanaoshindwa kurejesha mikopo kwa wakati, wamejikuta mali walizoweka kama dhamana zikitaifishwa na kuuzwa katika mazingira yasiyotoa fursa kuweza kupinga uuzwaji wa mali zao hizo.
Taasisi ya mikopo yaeleza
Mtendaji wa Kampuni ya Jojo Microfinance iliyopo Pugu Bombani, Alice Zebedayo alisema unapotaka kuchukua mkopo huo lazima ununue fomu kwa Sh5,000 kwanza ili usajiliwe kisha hatua zifuate.
Akizungumza na Mwananchi, Alice alisema fomu hiyo ikisharudishwa anayekopa anatakiwa atoe Sh5,000 nyingine ili viongozi wa kampuni hiyo wanapokwenda kumtembelea nyumbani kwake waangalie samani za ndani vitakavyowekwa dhamana ya mkopo husika.
“Kama ukichukua Sh100,000 utapewa Sh90,000 baada ya kukatwa Sh5,000 ya fomu na Sh5,000 ya kukutembelea nyumbani kwako ili kuangalia vitu vitakavyowekwa dhamana; halafu riba ya mkopo ni Sh30,000, hivyo unatakiwa ulipe Sh130,000 kwa mwezi mmoja,” alisema Alice.
Akifafanua namna ya kulipa, alisema mtu anapochukua Sh100,000 kila siku anatakiwa kulipa Sh4,300, “na ndani ya mwezi mmoja awe amemaliza na akikosa siku moja kulipa faini ya Sh2000 itamhusu kwa kukiuka.
“Kwa anayechukua Sh50,000 atalipa Sh65,000 na riba na kila siku anatakiwa atoe rejesho la Sh2,200 na akikosa siku moja anatakiwa alipe faini ya Sh2,000 na inategemea, siku zikiwa yingi na hela hiyo inazidi kuwa kubwa.”
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464