WANAWAKE LYABUKANDE,SHINYANGA VIJIJINI WAFUNDWA UMUHIMU WA HAKI ZAO.


Na Ali Liyatwi

Wanawake  Kata ya Lyabukande wilaya ya Shinyanga,wamekumbushwa kuunda Jukwaa la Wanawake litakalotetea na kusimamia haki zao, ikiwemo upatikanaji mikopo ya asilimia kumi kutoka fedha za ndani za Halmashauri ya wilaya.

Hayo yalielezwa  na Mratibu wa Mradi wa Chukua Hatua Sasa: Zuia Ukatili, John Eddy kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Women Elderly Advocacy and Development Organisation ( WEADO ) lililo na Makao Makuu yake Manispaa ya Shinyanga, linalotekeleza Mradi huo chini ya ufadhili wa WFT - Trust.

Eddy alisema uwepo wa Jukwaa hilo itasaidia kwa kiwango kikubwa kutetea haki mbalimbali za wanawake na kuondoa unyonge wa masuala mbalimbali mtambuka na kukuza uchumi wa familia zao 

Jukwaa hilo litafuatilia kama fedha za asilimia kumi kutoka Halmashauri Kama zinawafikia walengwa kwa wakati  ili kukuza uchumi wa familia zao",alisema Eddy

Aidha alisema uwepo wa jukwaa hilo utasaidia mapambano ya kutokomeza Ukatili wa kijinsi na kijinsia katika ngazi za familia hivyo kusababisha uwepo wa upendo utakaozalisha ushirikiano  katika familia na kuleta matokeo chanya katika jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa WEADO, Eliasenyi Nnko,alisema lengo la Mradi huo wa miezi mitatu ni kuielimisha jamii kuondokana na vitendo vya Ukatili ambavyo vimekuwa havina afya katika jamii 

Nnko alisema vitendo hivyo hususani vya ndoa za utotoni vimekuwa sababu ya kukwamisha uchumi wa nchi kutokana na kuondosha ndoto za vijana ambazo pengine Kama zingetimizwa zingelisaidia Maendeleo ya Taifa.  

Nae Mratibu wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ( MTAKUWWA) katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Aisha Omari, alisema Ni vyema kujitokeza kwa wadau mbalimbali  kusaidizana na Serikali kuielimisha jamii kuondokana na Ukatili wa kijinsia 

WEADO inatekeleza Mradi huo kwa kipindi Cha miezi mitatu katika kata ya Lyabukande Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ili kuhakikisha inaleta matokeo chanya dhidi ya Ukatili wa Kijinsia








 Mkurugenzi wa WEADO, Eliasenyi Nnko akitoa mafunzo kwa wakazi wa kata ya Lyabukande




Mratibu wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ( MTAKUWWA) katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Aisha Omari akizungumza na wananchi juu ya juhudi za wadau katika mapambano dhidi ya ukatili.

Watoto wa kata ya Lyabukande walioshiriki katika jukwaa hilo la kupinga ukatili wa kijinsia


Wanaume wa Kata ya Lyabukande walioshiriki katika elimu ya kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia





Mratibu wa Mradi wa Chukua Hatua Sasa: Zuia Ukatili, John Eddy kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Women Elderly Advocacy and Development Organisation ( WEADO ) akitoa elimu kwa wakazi wa kata ya Lyabukande.


Mratibu na Mkurugenzi wa shirika la WEADO wakiendelea kuelimisha wakazi wa kata ya Lyabukande



Mmoja ya wanawake wa kata ya Lyabukande akichangua hoja katika mkutano 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464