JUMUIYA YA WAZAZI CCM MKOA WA SHINYANGA YAPATA VIONGOZI WAPYA


Mwakilishi  nafasi ya mjumbe  wa baraza  kuu  na mkutano mkuu  CCM taifa Edward Nyakanyenge.

Na Kareny  Masasy, Shinyanga

JUMUIYA ya wazazi   ya chama cha Mapinduzi (CCM )mkoa wa Shinyanga imepata mwenyekiti mpya  John Siagi  ambaye amechaguliwa na wajumbe  kwa kupata kura  332 nakumshinda aliyekuwa akitetea kiti chake Salim Simba aliyepata kura 160.

Akitangaza matokea hayo  jana   msimamizi mkuu wa uchaguzi huo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga amemtangaza mwakilishi  nafasi ya mjumbe  wa baraza  kuu  na mkutano mkuu  CCM taifa Edward Nyakanyenge.

Kiswaga amewatangaza pia wajumbe  wa  uwakilishi wa nafasi mbalimbali  ambao  ni Agness  Kahabi  ambaye anawakilisha  wazazi kwenda  Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT).

Kiswaga alimtangaza James Jumbe aliyepata   nafasi ya  uwakilishi  kutoka kundi la wazazi kwenda  jumuiya ya umoja wa vijana UVCCM  mkoa.

Kiswaga amewatangaza  pia Veronica Nduta  kuwa mwakilishi  kutoka wilaya shinyanga vijijini, Juma Rajabu  mwakilishi kutoka Kishapu na Veronika  Mwayego kutoka Shinyanga mjini.

Mwenyekiti wa muda wa uchaguzi huo  Benard Shigela  amesema uchaguzi umefuata kanuni na sheria za chama  hivyo umekwenda kihalali.

Aliyekuwa mwenyekiti wa wazazi mkoa  Salim Simba amesema amekubali matokea na kumtaka mshindi  pale atakapo kwama asisite kwenda kwake kuomba ushauri.

Mwenyekiti aliyechaguliwa kwenye mkutano huo John Siagi amesema atahakikisha  anafika kwenye matawi kujua changamoto zao na kushirikiana  kwenye kila hali,

Katibu  ya jumuiya ya wazazi Regina Ndulu akitoa muongozo baada ya uchaguzi kuisha

Mjumbe wa  kamati ya siasa wilaya ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akitangaza matokeo



Washindi wa wakilishi kwenye  wilaya za Kahama,Shinyanga mjini,Shinyanga vijijini na Kishapu




Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi John Siagi  akitoa hotuba yake ya kuahirisha mkutano 




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464