KATIBU WA CCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI AMUOMBA DC KUWASWEKA NDANI WANAOHUJUMU RASILIMARI ZA MIRADI YA MAENDELEO BILA KUJALI ITIKADI YA CHAMA


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa majembe kwa wananchi wa Kijiji cha Bushola iliyoandaliwa na Sungusungu

Suzy Luhende,Shinyanga Blog

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Majeshi Ally Majeshi  amemuomba mkuu wa wilaya ya Shinyanga kuwakamata na kuwasweka ndani watu wanaohujumu miundombinu na rasilimali za miradi ya maendeleo inayotengenezwa na  serikali kupitia irani ya CCM.

Hayo ameyasema wakati akizungumza kwenye hafra ya kugawa mbegu za mahindi zenye thamani ya Sh  7,970,000 na majembe yenye thamani ya Sh 3,770,000 ikiwa ni pamoja na kuzindua ofisi ya serikali ya kijiji na ofisi ya jeshi la Sungusungu iliyoandaliwa na jeshi hilo la kijiji cha Bushola kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga na kufanyika katika kijiji hicho.

Majeshi amesema kuna watu ambao wapo ndani ya chama cha mapinduzi CCM lakini wanahujumu miundombinu mbali mbali ya kijiji na kuiba raslimali za serikali, watu hao wanatakiwa wakamatwe mara moja na kuswekwa ndani hawafai kabisa kuachwa waendelee kufanya maovu na kurudisha nyuma jitihada za serikali.

"Nakuomba mkuu wa wilaya kwa sababu wewe ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama usiwafumbie macho watu kama hao, kamata Sukuma ndani na mimi nipo nyuma yako nitawaunga mkono ili kuhakikisha maovu kama haya hayaendei,"amesema Majeshi.

Aidha amesema kuna watu wamezoea kuzunguka nyuma pale fedha za serikali zinapoletwa kwa ajili ya kufanya maendeleo wasitegemee kuwa kwa kuwa wako ndani ya chama wataachwa wote hao wachukuliwe hatua za kisheria kupitia mamlaka uliyonayo wanasababisha watu kupoteza amani kwenye CCM na serikali.

Pia amewapongeza viongozi wa sungu sungu kwa kufanya kazi nzuri na kubwa ya kuhakikisha  kuna usalama, kufanya maendeleo mbalimbali likiwemo la kujenga ofisi na ofisi ya serikali ya kijiji,  hivyo hata majirani kama kata ya Old shinyanga wanatakiwa kuiga ili kuondokana na uhujumu wa miundo mbinu na rasilimali za serikali na kulinda miundombinu iliyopo.

Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko aliwapongeza sungusungu kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuunga mkono jitihada za serikali kwa vitendo tena kwa kasi kubwa, ambapo inaonekana watafanya mambo makubwa katika kijiji hicho.

"Kwa kweli sina budi kuwapongeza kwa kazi kubwa mliyoifanya wanasungusungu wa Bushola mmekuwa watu wa mfano na wa kuigwa,nimekiwa nikiwatembelea kwa nyakati tofauti kwa ajili ya kuweka ustawi uliobora katika vikundi tulivyovihamasisha likiwemo Fogho"nho la sungu sungu ambalo ni kama SACCOS,"amesema Masumbuko.

Naye mkuu wa wilaya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika siku hiyo Jasinta Mboneko aliwapongeza sana sungu sungu na wananchi kwa kazi kubwa wanazozifanya, ikiwa ni pamoja na serikali kwa ujenzi wa Ofisi ya kijiji ofisi ya sungusungu na Zahanati, hivyo changamoto za kwenda kutibiwa mbali zitaisha.

"Agizo la katibu wa Chama cha mapinduzi nitalifanyia kazi watu wanaofanya maovu tutawachukulia hatua kali za kisheria, pia huduma za zahanati zitaendelea serikali tayari imeleta mganga na wauguzi ikiwa ni pamoja na dawa zipo za kutosha, hivyo serikali ya mama Samia Suluhu ipo makini haina uongo yenyewe imenyooka kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi,"amesema Mboneko.

Aidha mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura amesema wametambua kazi waliyoifanya sungu sungu kwa kushirikiana na serikali ya kijiji hivyo ameamua kuwatunukia cheti cha pongezi kwa kazi nzuri waliyoifanya, hivyo amewashauri kufanya maendeleo makubwa zaidi.

Akisoma risala ya Sungusungu Mwalimu Sebastian Salamba amesema  kijiji cha Bushola kilianzishwa mwaka 1974 kikiwa na kaya 250 kwa sasa kina kaya 350 na wakazi 1822, wanaume kuanzia umri wa miaka 18 wakiwa 398 na wanawake 414, na wanaume kuanzia mwaka 1 _ 17  ni 519 na wanawake 491 na kijiji hicho kina vitongoji viwili, ambapo sungu sungu ilianzishwa mwaka 1982 kwa lengo la kulinda mali za wananchi.

"Kila kaya imegawiwa majembe mawili na mfuko miwili ya mahindi ya mbegu lengo la kujiunga na fogo"nho  ni kwa ajili ugumu wa maisha kwa wananchi wa kijiji cha Bushola ambapo pia tumekuwa tukikopesha asilimia 10 ya fedha na kurudisha baada ya miezi mitatu, ambapo kupitia kundi hilo tumefanikiwa kutoa michango mbalimba ya maendeleo inayohitajika katika jamii,"amesema Mwalimu Salamba


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa majembe kwa wananchi wa Kijiji cha Bushola iliyoandaliwa na Sungusungu


O
Mkuu wa wilaya  Jasinta Mboneko akizungumza kwenye hafla ya ugawaji mbegu za mahindi na majembe 


Kazi ikiendelea ya ugawaji mbegu za mahindi na jembe


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akiwa na katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga na viongozi mbalimba wa kata na vijiji


Kamati ya Sungusungu iliyoandaa hafla hiyo ikijitambulisha 
Wananchi wa kijiji cha Bushola wakisubiri kugawiwa mbegu za mahindi na Majembe


Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye hafla hiyo

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wlaya ya Shinyanga mjini Majeshi Ally akizungumza kwenye hafla hiyo


Mkurugenzi wa halmashauri ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo aliwaomba viongozi wa sungusungu kwa kushirikiana na serikali ya kijiji waendelee kufanya maendeleo makubwa zaidi ili kujiongea uchumi


Jeshi la Sungusungu wakicheza mbele ya mgeni rasmi

Madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakisakata rumba na wanakijiji 


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akilisakata rumba na wanakijiji wa Bushola

Kazi inaendelea ya ugawaji mbegu za mahindi na majembe ya kulimia kwa mkono

Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Lucy Enock akisalimia wananchi wa kijiji cha Bushola


Shangwe na nderemo zikiendelea kijiji cha Bushola



Ugawaji wa mahindi na majembe ukiendelea 
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464