Msajili msaidizi wa hati mkoani Shinyanga Emanuel Gwaltu akiwa katika zoezi la utoaji wa hati kwa wananchi wilayani Kahama.
Na Kareny
Masasy ,Kahama
KAMISHNA wa ardhi msaidizi mkoani Shinyanga Leo Komba amesema zoezi la ugawaji wa hati 500 kwa wananchi wilayani Kahama kupitia kliniki tembezi ya utoaji na ugawaji hati kwa wamiliki wa viwanja walioomba limeanzia wilayni humo.
Akizungumza leo tarehe 17/11/2022 kwenye eneo la shunu kata ya Nyahanga ambalo lina mradi wa ugawaji wa viwanja kamshina Komba amesema wananchi
walio wengi bado hawana muamko wa
kushughulikia hati za umiliki wa viwanja vyao.
Kamishna
Komba amesema wameamua kutoa huduma hiyo
kwa ukaribu nakuwataka wenye viwanja
vilivyopimwa tayari waje na nyaraka zao
watahudumiwa na kupata hati..
“Tumeanzia
wilaya ya Kahama na tunafanya kazi hii muda wa siku mbili na tukimaliza
tunahamia wilaya zingine tunataka kazi hii iwe endelevu”amesema Komba.
Msajili wa
hati msaidizi kutoka mkoani Shinyanga Emanuel Gwaltu amesema wamekuja kugawa hati ambazo ziko tayari na zimesajiliwa nakuwaeleza wananchi faida ya kumiliki hati
ya viwanja ni kupata mkopo kwenye taasisi ya fedha na kujinyanyua kiuchumi.
“Ninacho
washauri wananchi wazitunze hati zao vizuri
zitawasaidia katika masuala mengi pia walio na viwanja wavisajili viwanja
vyao kwa kupata hati miliki ya kudumu”amesema
Gwaltu.
Japheti Kaliua na Hawa said wamesema wamefuatilia hati zao kwa muda mrefu lakini sasa zoezi walilolianzisha kuwafuata wananchi litaondoa urasimu wa kuzungushwa kwa kupigwa tarehe hivyo wamefurahi.
Maafisa ardhi wakiwa katika viwanja vya ofisi ya mtaa wa Shunu wilayani Kahama wakitoa hati kwa wananchi waliokuwa wameomba.
watumishi wa ofisi ya ardhi mkoa wa Shinyanga wakijiandaa na kazi
Kamishna msaidizi wa ardhi kutoka mkoani Shinyanga Leo Komba akiwa kwenye zoezi la ugawaji wa hati kwa wananchi wilayani Kahama.
Kamishna msaidizi wa ardhi kutoka mkoani Shinyanga Leo Komba akiwa kwenye zoezi la ugawaji wa hati kwa wananchi wilayani Kahama.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464