Mwenyekiti mpya wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Clement Madinda akiwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu(hawapo pichani) baada ya kumchagua kuwa mwenyekiti mpya.
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mkutano mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga umemchagua Clement Osward Madinda kuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoa huo baada ya kupata kura 240 huku akiwashinda washindani wake Pius Mwandu ambaye amepata kura 153 huku Jackline Ndombile akipata kura 11.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Lupakisyo Kapange amesema wajumbe walioshiriki katika uchaguzi huo walikuwa 413 kutoka wilaya za Kahama,Shinyanga na Kishapu walioshiriki katika kuwachagua viongozi hao.
Amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na haki ambapo wagombea wote walipatiwa haki ya kujieleza na kisha kuulizwa maswali na wajumbe ambao wamepata haki ya kikatiba ya chama hicho ya kumchagua kiongozi wanayemtaka.
Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika nafasi hiyo Clement Madinda aliwashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kumpa ridhaa ya kushika nafasi hiyo huku akiwataka wajumbe hao kudumisha umoja na mshikamano hali itakayo saidia kuimalisha ujenzi wa chama hicho.
“Uchaguzi umekwisha niwaombe vijana wenzangu tuwe wamoja ili kuhakikisha CCM inaendelea kusonga mbele katika kuliongoza taifa la Tanzania,niwaahidi nitakuwa kiongozi wa wote,” amesema Madinda.
Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Donald Magesa amewataka vijana kuvunja makundi baada ya uchaguzi kumalizika kwani CCM ina imani nao katika ujenzi wa chama hivyo ni wakati wa kushikamana katika kukilinda na kukitetea chama.
“Demokrasia mliyoionesha hapa inaonesha mmekomaa kisiasa kwani ingekuwa kwa vyama vingine wangeanza kupigana baada ya matokeo kutangazwa, CCM tunautaratibu mzuri wa kupangana katika nafasi za uongozi niwaombe muwe kitu kimoja,”amesema Magesa.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Lupakisyo Kapange akitangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa Jumuia ya vijana ambapo amemtangaza Clement Madinda kuwa mwenyekiti mpya
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Clement Madinda akiteta jambo na Mwenyekiti mstaafu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kulia).
Mjumbe baraza kuu UVCCM Taifa na mjumbe mkutano mkuu CCM Taifa Monalisa Daniel aliye washinda wapinzani wake baada ya kupata kura 304
Mjumbe baraza kuu UVCCM Taifa na mjumbe mkutano mkuu CCM Taifa Monalisa Daniel akiomba kura
Katibu Wa CCM mkoa Donald Magessa akitoa maelekezo ya uchaguzi.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi Kipange akitoa maelekezo ya uchaguzi kwa wajumbe na wagombea.
Wajumbe wakisubiri kupiga kura.
Kabla ya uchaguzi kuanza wagombea wanafarijiana.
Zoezi la kupiga kura linaendelea
Zoezi la kupiga kura linaendelea
Zoezi la kupiga kura linaendelea
Aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akiwaaga wajumbe wa mkutano mkuu ili kupisha uchanguzi mkuu wa mwenyekiti mpya
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464