Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu Linno Mwageni akiwa na makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwenye kikao cha kawaida cha baraza la amdiwani wakisikiliza hoja.
Na Kareny Masasy,Ushetu
BAADHI ya madiwani wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameomba wakulima kusogezewa mbolea ya ruzuku karibu na maeneo yao ili kuepuka gharama kubwa ya kusafiri kufuata mboleo hiyo kwa mawakala.
Wakiongea
kwenye kikao cha kawaida cha baraza la
madiwani hapo jana diwani viti maalum
Felister Kabasa na diwani wa kata ya
Mapamba Yohana Emanuel walitoa hoja hiyo.
“Mbolea ya ruzuku imekuja lakini
wakulima wanapata changamoto ya kuifuata
wanaiomba serikali kuliangalia hilo limeanza kuwakatisha tamaa wakulima”amesema diwani Kabasa.
Makamu
mwenyekiti wa halmashauri hiyo Doa Limbu
amesema changamoto ya umbali kufuata
mbolea za ruzuku na ucheleweshaji wa mbegu za pamba ufanyiwe kazi kwani kilimo ni sasa na izingatiwe idadi.
Ofisa kilimo
wa halmashauri hiyo Deus Kakulima
amesema wameongea na mawakala wanaotoa mbolea hiyo nakukubaliana kusogea karibu kuwe na vituo sita.
Madiwani hao wamelalamikia pia kushindwa kufanyika shughuli za maendeleo katika robo mbili za mwaka kutokana na mfumo wa kuhamisha fedha kushindwa kufunguka.
Diwani kutoka kata ya Kisuke Joseph
Bundala na diwani kutoka kata kinamapuka Samweli Sharifu walitoa hoja
hiyo katika kikao Cha baraza la madiwani.
Makamu
mwenyekiti wa halmashauri hiyo Doa Limbu amesema wamekuwa wakihitaji
maendeleo lakini suala la mfumo limeonekana kukwamisha na liko nje
ya uwezo wa halmashauri.
Mwekahazina wa halmashauri hiyo Prosper Mlacha amesema hakuna mfumo wa halmashauri ya Ushetu bali mfumo huo unatumika kwa nchi nzima na unasimamiwa na Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) na umekuwa ukileta changamoto .
Madiwani wa halmashauri ya Ushetu wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwaniMkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu Linno Mwageni akijibu hoja kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464