Meneja ofisi ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya ziwa Mwanza Musa Kuzumila akitoa taarifa za majitope ya bwawa la mgodi wa almasi wa WDL
Suzy Luhende, Shinyanga Blog
Meneja ofisi ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya ziwa Mwanza Musa Kuzumila amesema wamefanya upimaji wa maji na tope ya bwawa lililopasuka la mgodi wa almasi wa Williamson Diamond Ltd (WDL) na kukuta kwamba maji hayo hayana madhara kwa binadamu na wanyama, hivyo wananchi wanaruhusiwa kutumia na kunywesha mifugo kama kawaida.
Hayo ameyasema leo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo amesema wamefanya upimaji wa maji na tope na kuonekana hayana madhara ya aina yeyote, hivyo wananchi waondoe hofu waendelee kutumia maji hayo.
"Tulianza upimaji wa sampuli tarehe 9mwezi huu baada ya tukio hili kutokea tulipima maji na tope ambapo tulichukua maji magarbi mwa bwawa la almas na upande wa kwenye vijiji vilivyoathirika, hivyo tulibaini tope na maji hayana kemikali ya aina yoyote, maji hayo yapo salama hivyo tunawaomba wananchi wasiwe na hofu tena,"amesema Kuzumila.
Kwa upande wake meneja NEMC kanda ya ziwa mwanza Jarome Kayombo alisema kuna uchunguzi mbalimbali umefanyika kuhusiana na bwawa hilo kupasuka ofisi ya mkemia wamepima wameona maji hayo hayana madhara kwa wananchi na kwa wanyama.
Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema alisema baada ya bwawa kupasuka maji kutiririka wananchi walishindwa kutumia maji kwa kuhofia yana madhara, lakini vipimo vimeonyesha maji haya ni salama, hivyo wanatakiwa kutumia bila wasiwasi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude alisema taharuki kwa wananchi wa Wilaya ya Kishapu ilikuwa kubwa lakini kwa sasa wataalamu wametangaza maji hayo hayana madhara waendelee kutumia na kunywesha mifugo.
" Tume tuliipa siku saba kwa ajili ya uchunguzi kwa ajili ya unyeti wa utaalamu na taarifa ya awali sasa wananchi wasiwe na hofu tena maji hayo yamepimwa hayana madhara, hivyo kuna uhakika hivyo waendelee kutumia tu bila hofu, na tume tumeiongezea muda wa kufanya uchunguzi zaidi mpaka tarehe 20 mwezi huu,"alisema Mjema.
"Baada ya bwawa la majitope kubomoka taharuki ilikuwa kubwa, kwamba maji hayo siyo salama lakini leo nafarijika kudikia kwamba maji hayo hayana madhara, nashukuru kwa kutangaziwa na mkuu wa mkoa pamoja na mkemia mkuu wa serikali, hivyo wananchi wangu wasiwe na wasi wasi tena maji ni salama kabisa,"alisema Mkude.
Kwa upande wake meneja NEMC kanda ya ziwa mwanza Jarome Kayombo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza
Viongozi mbalimbali wakisikiliza taarifa ya mkemia mkuu wa serikali akitoa taarifa
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464