MRATIBU WA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO SHINYANGA AWATAKA MAAFISA WANAOJIHUSISHA NA KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Monica Venance Sehere 

Suzy Luhende, Shinyanga  Blog

Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Monica Venance Sehere amewataka maafisa wanaoshughulika na kesi za watu wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia wasifanye kazi zao kwa mazoea badala yake wafanye kazi kwa weledi na kwa tija katika kusimamia haki za wananchi.

Hayo ameyasema leo wakati akifunga mafunzo kazini kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi na Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto leo Novemba 21,2022, 
ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT) ambapo amewataka kuzingatia maadili ya kazi zao.

Monica amesema  maa afisa wote wa jeshi la polisi wanaohusika na mambo ya upelelezi ni  vizuri wakawasikliza kwa umakini watu wanaokuja ofsini na malalamiko wasikurupuke tu,  pia  washirikiane na polisi kata kwa sababu wanawajua watu wao wanaoishi nao, kwani wakiwaacha mbali hawatapata ushirikiano mzuri wa kuwasaidia wananchi.

"Pia tunapokuwa tunaendelea na shughuli zetu za kiupelelezi tusiwasahau watendaji  wa kata tuwatumie tusitegemee sana madaktari kwa sababu nao  ni binadamu, dawati la jinsia linatakiwa kutekeleza majukumu yao ili kuondoa changamoto, tutekeleze majukumu yetu ipasavyo,"amesema Monica.

Pia alisisitiza kuwa wanaposimamia kesi za ubakaji na kufikia hukumu wawe wanafuatilia kwa sababu inafikia wakati huyo aliyetenda kosa anahukumiwa miaka 30,  lakini akija kukata rufaa anatoka na kuanza kujitapa nakutamba kwenye jamii, hivyo kesi hizo ziwe zinafuatiliwa ili kuhakikisha mlalamikaji anatendewa haki.

"Sisi kweli tuna mapungufu yetu na mahakama wana mapungufu yao kwa sababi nao ni binadamu, tujitahidi tu kufuatilia ili kuwatendea haki watendewa, na tunapofanya shughuli zetu lazima tuwe wasiri "amesema Monica mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa Shinyanga.

Sheila Zongo mpelelezi wa mkoa akizungumzia masuala ya sheria ya mtoto amesema watoto wengi wanajikuta wanashawishika na kuingia  kwenye zinaa kwa sababu ya tamaa, hivyo wazazi wahakikishe wanawapa watoto wanachohitaji ili kuondokana na changamoto hizo.

"Ili kuondokana na changamoto za watoto wetu kupata tamaa, wazazi tuwape mahitaji wanayohitaji na tuwe marafiki wa watoto wetu, tuwakague mara kwa mara wanaporudi majumbani  ili kutokomeza mambo ya ukatili kwa sababu waharifu tunao na tunaishi nao kwenye jamii yetu,"amesema Sheila.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Masudi Najim ambaye pia ni afisa wa polisi amesema wapelelezi wanapofanya uchunguzi kwa mtu aliyefanyiwa ukatili wazingatie mambo yote waliyofundishwa, kwani wakizingatia lazima ushahidi unajionyesha hata kama mashahidi wakikana ukifuata vigezo vyote ushahidi unakamilika.

Kwa upande wake mkuu wa zahanati ya polisi Bibititi Mohamed amesema kweli wanawake wanapeleka malalamiko katika dawati la jinsia  lakini wanatakiwa wanatakiwa kusikilizwa mme na mke kwani wanaume wengi wamekuwa wahanga wa kunyanyaswa na wake zao, unakuta mwanamke mwenyewe kafanya kosa halafu anawahi dawati la jinsia.

"Mwanamke anapofanya kosa na kukimbilia dawati la jinsia na mwanaume kukamatwa na kuwekwa ndani inamsababishia mwanaume kuwa na msongo wa mawazo na kusababisha wengine kujinyonga, hivyo ni vizuri kusikiliza pande mbili ili hata akionekana mwanamke ni shida wanashauriwa,"amesema Bibititi.

Maafisa wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo kuzuia ukatili w kijinsia


Masudi Najim ambaye pia ni afisa wa polisi ambaye alikuwa akofundisha jinsi ya kupata ushadi wa mwili na wa nuwele









Bibi titi Mohamed mkuu wa zahanati ya polisi


Sp Militon Tandali akizungumzia sheria mbalimbali
Sheila Zongo mpelelezi wa mkoa akifundisha sheria za mtoto


Kaika Desideri afisa wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga





Semeni Gaudence Nzigo inspecter akizungumzia sheria ya ndoa


Jeremia Siitta kitengo cha kitengo cha mifugo mkoa wa Shinyanga


Richard Kapongo mkaguzi wa polisi mkoa wa Shinyanga akichangia jambo

Abasi Mushi afisa wa polisi ambaye alikuwa mwezeshaji




Masudi Najim ambaye pia ni afisa wa polisi ambaye alikuwa akofundisha jinsi ya kupata ushadi wa mwili na wa nuwele
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464