Jamii imetakiwa kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia kutokana na kuishi nao kwenye jamii ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekuwa ni changamoto kubwa kwenye jamii na kusababisha baadhi ya watoto kushindwa kupata elimu.
Hayo
yameelezwa na Mwenyekiti wa kikundi cha Sauti ya Mama kutoka Jijini Dar es
salam Samila Rashid ambao ni wasanii wa filamu wakati wakitoa elimu ya ukatili
wa kijinsia juu ya kupinga mimba na ndoa
za utotoni pamoja na elimu kwa vijana kwenye shule za msingi na sekondari
Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na taasisi ya Holy Smile yenye makao
makuu yake Mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti
wa Sauti ya mama amesema kuporomoka kwa maadili katika jamii ni chanzo cha
matukio mengi ya ukatili wa kijijinsia kwa watoto vikiwemo vitendo vya ubakaji
na kulawiti hali ambayo inatakiwa kukemewa vikali na wadau wa kupinga ukatili,jamii
na serikali.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Holy smile Arnold Bweichum amesema katika
kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia wameamuwa kushirikiana na Sauti
ya mama kutoa elimu mashuleni juu ya kupinga vitendo hivyo.
Amesema
wametoa elimu katika shule tano za Mkoa wa Shinyanga ili kuwawezesha wanafunzi
kutambua athari za ukatili wa kijinsia na kujua namna ya kujiepusha na vitendo
hivyo ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo yao.
Amesema
kampeni hiyo ya kutoa elimu mashuleni ni mwendeleo ili kuhakikisha watoto na
jamii nzima inapata uelewa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464