Shirikisho la watu wenye ulemavu mkoa wa Shinyanga (SHIVYAWATA) limeiomba serikali kufanya ukaguzi wa mifumo ya miundombinu ya umeme katika mabweni ya shule ya Msingi Bungangija mchanganyiko ili kudhibiti majanga ya moto.
Ombi hili
limetolewa na Mwenyekiti wa SHIVYAWATA mkoa wa Shinyanga Gerald Mpongo
katika zoezi la kuaga miili ya wanafunzi watatu walipoteza maisha Novemba 24
mwaka huu baada ya kuungua moto bweni walilokuwa wamelala katika hospitali ya
rufaa ya mkoa huo.
Amesema kuwa
ipo haja kwa serikali kuhakiki mifumo ya umeme katika mabweni na madarasa ya
majengo ya shule hiyo ambayo yalijengwa muda mrefu ili kukabiliana na majanga
kama vile moto ambao umesababisha wanafunzi watatu wenye ulemavu wa macho
kupoteza maisha wakiwa wamelala.
“Serikali
kupitia shirika la umeme Tanzania (Tanesco ) mkoa wanatakiwa kukagua mifumo
hiyo ikiwezekana kuibadilisha kwani iliyopo imeshachakaa kutokana na kuwekwa
muda mrefu,na itasaidia kuongeza ufanisi wa kuzuia majanga ambayo yanaweza kuzuilika,”amesema
Mpongo.
Sambamba na
hilo Mpongo aliomba serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo,
ili wazazi na walezi wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho wasieendelee kuwa
na hofu juu ya usalama wa watoto wao katika kituo hicho.
Kwa upande
wake Shekh wa wilaya ya Shinyanga Sudi Katengire aliwaomba wazazi na walezi
kuwa watulivu wakati serikali ikielendelea na uchunguzi wa tukio hilo na
kuwaomba kuendelea kuwaombe kwa Mungu watoto waliotangulia mbele za haki.
Awali akitoa
salamu za serikali mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema alisema kuwa
tayari serikali imekwisha chukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kumwagiza
mkuu wa jeshi na zimamoto kuhakikisha wnafanya uchunuzi wa tukio hilo pamoja na
kutoa elimu ya kukabiliana na majanga kwa wanafunzi.
“Serikali imegharamia mazishi ya wanafunzi hawa,tunatoa pole kwa wazazi waliowapoteza watoto wao kuhusiana na janga la moto ,sisi kama serikali tunaendelea na uchunguzi wa tukio hili ili kubaini chanzo chake niwaombe muwe watulivu,”amesema Mjema.
Mwenyekiti wa Shivyawata mkoa wa Shinyanga Richard Mpongo akielezea namna walivyoguswa na msiba huo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464