Mwandishi wetu.
Mtandao wa asasi za kirai mkoa wa shinyanga unaopamba na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga(SHY-EVAWC) umeratibu mafunzo ya siku mbili mkoani Shinyanga kwa asasi zinazopamba na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mtandao huo wa kutokomeza ukatili mkoa wa Shinyanga( SHY-EVAWC) umefanya mafunzo ya kuongeza uelewa kwa wanachama wake wake wapatao 28,katika ukumbi wa karena hotel manispaa ya Shinyanga ,leo jumanne 15 Novemba,2022.
Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na TAPO La SHY-EVAWC kwa ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT-T) ulilenga kukutanisha asasi za kirai kwa malengo ya kupanua uelewa kwa wadau wanaopinga ukatili kwa agenda ya ufeminia,kanuni na mikakati ya kuimarisha nguvu za pamoja(TAPO).
Pia kusaidia wadau wanaopinga ukatili kubaini maeneo ya kijinsia yenye changomoto za ukatili na kupendekeza mbinu za kuimarisha uchopekaji wa kanuni za kifemia miongoni mwa wana TAPO( wadau wanaopinga ukatili) na kutengeneza njia bora na mikakati ya kuwa naTAPO imara la kifeminia.
Jonathan Kifunda ambaye ni Mwenyekiti wa TAPO la SHY - EVAWC alisema mafunzo haya ni muhimu kusaidia kuboresha shughuli zetu kwa kazi tunazofanya dhidi ya kupambana na ukatili.
"TAPO letu ni jukwaa muhimu sana na serikali yetu imekuwa ikitumia jukwaa hili kwa kupitia ngazi mbalimbali katika kutafuta mikakati na kupata maoni ya mipango madhubuti ya kusaidia kutokomeza ukatili kwa ngazi ya mkoa na taifa,viongozi wengi wameshatufikia na kufanya nao majadiliao ya kuweza kutokomeza ukatili "Alisema Jonathan
Kwa upande wake,Rebecca Mjema ,Mwezeshaji alisema tumeitana hapa ili kuwa na malengo endelevu kwa kuwa na mipango na mikakati ya kutokomeza ukatili.
John Eddy mwakilishi wa Shirika la WEADO alisema kuwa mafunzo haya ni muhimu kwa kumsaidia kuongeza uelewa zaidi katika eneo la ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Washiriki kutoka asasi za kiraia mkoa wa Shinyanga wakiwa katika mafunzo ya ufeminist na Nguvu ya TAPO.
Washiriki wa mafunzo wakisikiliza mwezeshaji.
Mwenyekiti wa SHY- EVAWC ,Ndugu Jonathan Kifunda akifungua semina ya mafunzo.
Rebecca Mjema Kisenha ,Mwezeshaji wa dhana ya ufeminist akizungumza.
Wadau wa kupinga ukatili mkoa wa Shinyanga wakiwa katika mafunzo.