Watumishi wa mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa kikodi Kahama wakiwa ofisini kwao wakijiandaa kwa kutoa msaada,
Mwakilishi
wa kamishna mkuu wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kutoka makao
makuu Ndositwe
Haonga amewaongoza watumishi wa mamlaka hiyo
wa mkoa wakodi Kahma kutoa msaada
kwa wafungwa.
Msaada huo ni Kandambili,,Sabuni,taulo za kike, dawa za meno na Miswaki.
Akitoa
msaada huo kwa mkaguzi msaidizi wa
gereza wilayani Kahama Anastazia Mwamlima leo tarehe 27/Novemba/2022 katika maadhimisho ya
shukrani kwa mlipa kodi.
Haonga
amesema upo utaratibu wa kurudisha shukrani kwa walipa kodi hivyo watatembelea kwenye makundi maalumu
kama vile Magereza na watoto yatima kutoa msaada.
“Pia siku ya
kesho tunatarajia kutoa tuzo kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa walipa kodi
wazuri hilo ni jukumu letu….”amesema
Haonga.
Meneja mkoa
wa kodi Kahama Warioba Kanile amesema
wameamua kutoa shukrani kwa njia hiyo
hivyo makundi maalumu yatapokea msaada huo lengo kudumisha mahusiano na jamii nakuwataka
walipe kodi kwa mujibu wa sheria.
Akipokea
msaada huo Mwamlima kwa niaba ya mkuu wa gereza
la wilaya hiyo Hamza Abdala ameshukuru
kwa msaada huo kwani wafungwa wengine hawana ndugu wa kuwapatia na huo ndio
utakuwa msaada kwao.
“Hapa tunawahifadhia wafungwa pindi wakiwa na shida wamekuwa wakitufuata nakuwaeleza shida waliyonayo hivyo watasaidiwa kupitia vifaa hivi”amesema Mwamlima
Mwakilishi wa kamishna mkuu wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kutoka makao makuu Ndositwe Haonga wa pili kutoka kushoto akiwa na meneja wa mkoa wa kikodi Kahama Warioba Kanile aliyevaa kofia,
Baadhi y watumishi wa mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa kodi Kahama wakiwa eneo la gereza wilayani Kahama
Mwakilishi wa kamishna mkuu wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kutoka makao makuu Ndositwe Haonga akizungumza walivyoguswa kutoa msaada kwa wafungwa katika gereza la wilaya ya Kahama
Mkaguzi msaidizi wa maregeza ya wilaya Kahama Anastazia Mwamlima akisalimiana na maafisa wa TRA.
Meneja wa mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa kikodi Kahama pamoja na Mwakilishi wa kamishna mkuu wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kutoka makao makuu Ndositwe Haonga wakisalimiana na mkuu wa gereza wilaya ya Kahama Hamza Abdallah.
Mwakilishi wa kamishna mkuu wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kutoka makao makuu Ndositwe Haonga akisalimiana na mkaguzi wa gereza Anastazia Mwamlima.
Watimishi wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa kodi Kahama wakiwa eneo la ofisini
Watumishi wa mamlaka ya mapato TRA mkoa wa kikodi Kahama wakijiandaa na utoaji wa msaada.