MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kikodi Kahama wakiwa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya shukrani kwa mlipa kodi pamoja na baadhi ya wafanyabiashara.
Na Kareny
Masasy, Kahama
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kodi Kahama umejivunia kuvuka lengo kwenye ukusanyaji wa mapato kwa kipindi kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba mwaka 2022.
Meneja mkoa wa kikodi Kahama Warioba Kanile amesema
hayo leo tarehe 28/Novemba/2022 katika
kilele cha maadhimisho ya shukrani kwa mlipa kodi yaliyohudhuliwa na
wafanyabiashara huku mgeni rasmi akiwa mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga.
Warioba
amesema maadhimisho hayo yamekwenda na ujumbe unaosema “Asante kwa kulipa kodi kwa ustawi wa jamii
na maendeleo ya Taifa -kazi iendelee” ikiwa makusanyo kwa kipindi
hicho walipangiwa lengo zaidi ya sh Billioni
5.9 na makusanyo yakawa zaidi y ash Billioni
7.1 ambayo ni ufanisi wa asilimia 119.71.
“Lengo la maadhimisho haya ni kutambua mchango na
ushirikiano uliopo baina ya TRA na wadau
wake na kupitia maadhimisho imekuwa ikiwaweka pamoja na wadau
kwa kushiriki katika shughuli
mbalimbali za kijamii,burudani na kupata mrejesho”amesema Kanile..
Mwakilishi
wa kamishna mkuu kutoka makao makuu TRA Ndositwe Haonga amesema Siku ya mlipa kodi ni siku
iliyotengwa rasmi kwaajili ya kutambua mchango inayotolewa na walipakodi katika ngazi zote hivyo
inawahusu wananchi wote.
Haonga
amesema dhamira ya siku ya mlipakodi ikiwa
ni ileile kwa kuamini kwamba kuna usimamizi mzuri wa kodi ndani ya nchi .
Haonga amesema ipo tija na ufanisi wa hali ya juu kwa
ushirikishwaji pamoja na kuchukua mawazo
na mapendekezo ya mlipa kodi katika kutunga sheria na sera za kodi,kujadiliana
juu ya mbinu na mikakati mbalimbali.
“Tunapowaenzi
walipakodi tunatambua kuwa hadhi yao imetoa mchango mkubwa katika kulinda uhuru
wa taifa pia kutambua wanaofanya vizuri inakuwa ni moja ya motisha muhimu ya
kuendeleza ufanisi”amesema Haonga..
Haonga
amesema wanafahamu wapo walipakodi wachache ambao wana ridhaa ndogo ya kulipa
kodi na wale ambao hawalipi kabisa kodi ambayo ni stahiki ya serikali wanatakiwa kubadilika na kuiga mfano.
“Katika
kutimiza hili TRA imedhamiria kuongeza
ukusanyaji wa mapato kwa kuimarisha
namna ya ukusanyaji,udhibiti wa mianya
ya upotevu wa kodi,kubainisha
vyanzo vipya vya mapato na kuweka mazingira rafiki kwa walipakodi nakuwa
na mifumo ya usimamizi wa kodi ili kurahisisha ulipaji kodi”amesema Haonga.
Mkuu wa
wilaya ya Kahama Festo Kiswaga amewapongeza
TRA kwa kutomuangusha kutokana na ukusanyaji mzuri wa mapato, ila
bado kuna changamoto ya wafanyabishara
kutotoa risti kwani anawashauri wakitoa
risiti hata mteja hasumbuliwi na kuweka kumbukumbu zao vizuri katika biashara.
“Wafanyabiashara
wapatiwe elimu mara kwa mara na
wachangie kimawazo walio wengi hawana
elimu na mashine za Kielektroniki (EFD)
hakuna budi kwenda na mabadiliko ya sasa mashine hizo zitaondoa changamoto zote walizonazo”.amesema
Kiswaga.
Kiswaga
amekabidhi vyeti vya utambuzi wa walipakodi katika makundi ya wafanyabiashara wadogo,wakati na wakubwa
ambapo zawadi ya ushindi wa jumla ilikwenda kwenye shirika la PANAFRICAN MINING SERVICES LTD
Mwenyekiti wa chemba ya biashara,viwanda na kilimo (TCCIA) Charles Machali amesema hivi sasa kuna uhai kati ya wafanyabiashara na TRA na ndiyo maana unaona biashara za ufunguzi wa maduka zimeongezeka wanachohitaji ni kupatiwa elimu zaidi.
Upande wa kushoto ni meneja kutoka mamlaka ya Mapato Tanzania mkoa wa kikodi Kahama Warioba Kanile akiwa na mwakilishi wa kamishna mkuu kutoka makao makuu Ndositwe Haonga.
Wadau wakiwa kwenye ukumbi wakisikiliza hotuba za mamlaka ya mapato TRA zikitolewa na maafisa wa mamlaka hiyo.
Kamti ya ulizi na usalama ya wilaya ya Kahama
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akimpatia cheti mmiliki wa shule za Rocken Hill na Anderleck alichopewa na TRA.
Mkuu wa wilaya Festo Kiswaga akiendelea kutoa vyeti kwa wafanyabiashara.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga naye akikabidhiwa cheti kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kikodi Kahama na mstahiki meya wa manispaa ya Kahama Yahya Bundala.
Wafanyabiashara wakisikiliza
Mwenyekiti wa TCCIA wilayani Kahama Charles Machali
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464