MAMLAKA ya
mapato Tanzania (TRA ) mkoa wa kodi Kahama
umetoa msaada vitu mbalimbali kwa watoto yatima 49 wanao lelewa kwenye kituo cha KAHAMA PEACE ORPHAN
CENTER.
Mkurugenzi
wa kituo hicho Halima Hamza amepokea
msaada huo leo tarehe 27/Novemba/2022 katika
maadhimisho ya siku ya shukrani kwa mlipa
kodi kutoka TRA huku akielezea changamoto ya kukosa mfadhili wa
kudumu.
Hamza ameeleza
idadi ya watoto alionao kuanzia umri wa
mwaka 0 hadi miwili idadi yao ni saba,
na wenye umri kuanzia miaka mitatu hadi
minane idadi yao ni 12 walio baki
idadi yao ni zaidi ya miaka 10.
Hamza
amesema changamoto kubwa waliyonayo kituoni hapo ni kukosekana mfadhili wa
kudumu nakukosa mahitaji ya muhimu kama chakula ikiwa watoto 28 wanashinda kituoni hapo mchana nakurudi
majaumbani mwao na watoto 21 wanalala kituoni hapo.
Hamza amesema
katika suala la matibabu baadhi watoto
wana bima za afya wengine hawana
wanatumia vibali maalumu vilivyotolewa na ustawi wa jamii kupitia dawati
la jinsia.
Msaada
ameupokea kutoka TRA ni mchele kilo 150, Maharage kilo 30, sukari kilo 40 , mafuta ya
kupikia ndoo mbili kubwa,maji katoni 10 ,sabuni katoni moja,mafuta ya
kupaka katoni tano, madaftri dazani mbili, kalamu za
wino boksi tano, Biskuti kopo kumi na juisi katoni 10.
Katibu wa
kituo hicho Shabani Mbwana amesema msaada huo wanashukuru una maana sana kwani watoto
wamepata faraja kwani wamekosa malezi na upendo wa karibu kama wanavyopata
watoto wengine majumbani.
Mwakilishi
wa kamishna mkuu kutoka makao makuu TRA Ndositwe Haonga amekabidhi msaada huo kwa kutoa shukrani kwa njia hiyo kuwakumbuka
makundi maalumu yenye uhitaji ikiwemo kituo cha kulelea watoto yatima.
“Wananchi
wanalipa kodi na shukrani yetu kwao
tunaitoa tunairudisha kwa jamii wenye uhitaji
ili watoto nao wajifunze namna ya kulipa kodi pindi wakiwa wakubwa” amesema
Haonga.
Meneja wa TRA mkoa wa kikodi Kahama Warioba Kanile amesema leo wameamua kutoa msaada wa vitu katika
makundi maalum kwa kile wanachokipata
kwa kuwashukuru walipa kodi na ujumbe wetu ni wananchi walipe kodi kwa hiari na wajibu wetu kuisaidia jamii hasa
makundi maalum.
Mwakilishi wa kamishna mkuu kutoka makao makuu TRA Ndositwe Haonga akiwa amembeba mmoja wa watoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima.
Maafisa wa TRA mkoa wa kikodi Kahama wakiwa wamebeba watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima.
Mwakilishi wa kamishna mkuu kutoka makao makuu TRA Ndositwe Haonga akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima
Mmoja wa maafisa kutoka TRA mkoa wa kikodi Kahama akiwa amebeba mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464